Takribani miezi mitatu imepita tangu Chidi Benz
azungumzie kuhusu harakati zake za kufanya album na mkali wa hip hop
Fid Q, Fareed vs Rasheed. Leo hii ameongelea alipofikia juu ya
kukamilisha album hiyo

Album
hiyo ambayo imetokana na idea ya Chidi Benz tayari imeshaanza kufanyiwa
kazi ambapo ngoma moja imeshakamilika lakini Chidi pia ameongelea
kuhusu yeye mwenyewe na ratiba ya kuingia studio.
"kwasababu tulisha record ngoma moja so nafkiri sasa, now tunatakiwa
tuingia mzigoni so nahisi the project itakuwa noma and me najitayarisha
kuingia ingia vistudio napitia vistudio viwili vitatu hapa na pale nini,
kwahiyo natafuta bado, nahisi nikijakupata msumari ntakuja tu kusema
jamani eeh baada ya huu ni huu sasa hivi niko nautengeneza tengeneza na
create," amesema Chidi
http://www.djfettytz.com/2014/08/audio-chidi-benz-kufanya-album-ya.html
Ya tunafanya album mzima inabidi tupge mikono tu, chidi na fid kwasababu ni Rasheed na Fareed kwahiyo tumeamua tu sisi wenyewe kufanya kitu..........
Ni idea yangu nilikuwanayo kabla sijatoa ngoma wala sikujua kama
nitakuwa busy na ngoma kwahiyo nilikuwa najua kwamba kwa kipindi ambacho
nitakuwa nimekaa nirecord project na Fid so ya imekuja imekuwa ratiba
imebaki pale pale tunafanya, tuna mpango tu wa kupiga ngoma za ajabu
sana." alimalizia Chidi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni