Marekani. Mwanamuziki Beyonce anafahamika kwa umahiri wake wa kuteka vyombo vya vya habari
wakati mwingine bila hata kufungua kinywa chake. Ndoa yake, ujauzito
wake na kuachia albamu kimyakimya ni mambo ambayo yamewahi kuvunja
rekodi za kuandikwa mara nyingi huku mwenyewe akibaki kimya.
Katika mahojiano na Jarida la Bazaar, ‘supastaa’
huyo anafunguka kuhusu upande mwingine wa maisha yake katika muziki,
fasheni na familia.
Bazaar: Kama ukipewa nafasi ya kurudi utoto ni kitu gani utafanya?
Beyoncé: Nitaiamuru nafsi yangu ijiamini. Sasa
hivi nimefikia katika hatua ambayo sijali watu wengine wanasema nini juu
yangu. Nilipokuwa mdogo kila nilichofanya kwanza nilitaka kujua, je,
watu watanichukuliaje.
Bazaar: Mara nyingi umekuwa ukisema wewe ni mtu mwenye aibu, lakini katika kazi zako unaonekana unajiamini, hii ikoje?
Beyoncé: Sasa hivi sina aibu sana kama ilivyokuwa
zamani. Mimi ni mtu ninayependa zaidi kusikiliza kuliko kuongea ndiyo
maana naonekana kuwa na aibu. Ninajiamini, ninapenda ninachofanya na
ninajituma haswa.
Bazaar: Unawataja Diana Ross na Tina Turner kama unafuata nyayo zao, kitu gani hasa unakipenda kutoka kwao?
Beyoncé: Walikuwa ni wanawake waliojituma bila waoga. Kumbuka pia wanawake hawa waliofanikiwa kuchomoza katika jamii ambayo ilikuwa ikimdharau mtu mweusi.
Bazaar: Uko karibu sana na mdogo wako Solange, lakini aina ya maisha yenu ni tofauti, ni kitu gani kinawaunganisha?
Beyoncé: Kwanza kama ulivyosema Solange ni mdogo
wangu. Ninampenda sana na nafikiri tofauti zetu katika mambo
tunayoyapenda na kuamini ndiyo inayotuunganisha.
Bazaar: Ushauri gani mzuri ambao mama yako amewahi kukupa?
Beyoncé: Amewahi kunipa ushauri wa aina mbalimbali
lakini bora kuliko wote ni kuhusu uzuri. Mama aliwahi kuniambia uzuri
wa nje huwa unachuja, lakini wa ndani unaishi milele. Mama yangu ni mtu
mwema na anayependa kujitoa. siku zote anatusisitiza katika kujitoa kwa
wengine.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni