Rapper aliekuwa anawakilisha Dirty South, Ahmed Ally Upete, a.k.a "Geez Mabovu" amefariki dunia jioni ya leo (November 11) mishale ya sa moja akiwa kwao mkoani iringa
Geez ameugua kwa muda mrefu na baada ya hali yake kuonekana sio nzuri
kaka yake alikuja kumchukua na kurudi nae mkoani Iringa, ameniambia
mdogo wake ambae pia ni msanii "Mad P" kupitia ujumbe mfupi wa maneno.
habari zaidi utaendelea kuzipata kila zinapotufikia
Mabovu alikuja juu sana baada ya kutoa ngoma inayoitwa Mtoto Wa Kiume na dakika sifuri aliyomshirikisha marehem Albert Mangwea.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni