ANA KWA ANA:Nakaaya - MKWELI BLOG

Karibu kwenye kitovu cha HABARI.

PATA HABARI ZA MICHEZO KUTOKA KILA KONA YA DUNIA NA MAGAZETI KWA WAKATI UKIWA KARIBU NASI

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Ijumaa, 7 Novemba 2014

ANA KWA ANA:Nakaaya



Umekuwa kimya kwenye muziki, kwa nini?
Miaka mitano iliyopita imekuwa na vikwazo vingi. Nililazwa kwa miezi nane baada ya kupata ajali mbaya ya barabarani, halafu nikapata ujauzito na kuanza kulea. Najua sasa unaelewa kwa nini nimekuwa kimya.
Kukukumbushia tu, uliwahi kuingia mkataba na kampuni ya kimataifa inayosimamia kazi za wasanii ya Sony baada ya kutoka Tusker Project Fame. Mkataba ule uliishia wapi?
Haukwisha vizuri, niliingia mkataba wa miaka mitano wakati nikiwa Denmark. Nilipewa kiasi kidogo cha fedha na huo ukawa mwisho wetu.
Ulipewa shilingi ngapi?
Nilipewa Dola 11,000 (Sh18.2 milioni).
Kwa maana hiyo Sony hawakukufuatilia tena?
Nilirekodi wimbo “Mr Politician” na ilibidi tugawane mapato. Hata hivyo, hawakunifuatilia tena na ikawa vigumu kutimiza makubaliano yetu ya awali.
Hiyo inamaanisha nini?
Nilikuwa na mkataba wa miaka mitano ambao unanifunga kufanya kazi na mtu mwingine yeyote. Kama ningejaribu kukiuka huenda ningeburuzwa mahakamani, hivyo ilibidi niishi hivyohivyo katika kipindi kile. Kilikuwa kipindi kigumu sana kwangu.
Ulishiriki mashindano ya kwanza ya Tusker Project Fame, je, kuna mshiriki yeyote ambaye unawasiliana naye mpaka sasa?
Siyo wengi, zaidi ya mshindi Valerie Kimani. Ni rafiki yangu wa karibu na wote hivi sasa ni wazazi tunaolea watoto bila baba zao. Mara nyingi tunaongea na kufurahi pamoja.






Hakuna maoni:

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Kurasa