Duma aingia ndani ya gari la watalii Serengeti, Tanzania - MKWELI BLOG

Karibu kwenye kitovu cha HABARI.

PATA HABARI ZA MICHEZO KUTOKA KILA KONA YA DUNIA NA MAGAZETI KWA WAKATI UKIWA KARIBU NASI

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Ijumaa, 30 Machi 2018

Duma aingia ndani ya gari la watalii Serengeti, Tanzania

Britton Hayes na mjomba wake, wote kutoka Seattle, Washington, walikuwa safarini kujionea wanyama katika mbuga ya taifa ya Serengeti nchini Tanzania pale duma huyu alipoanza kuwa mtalii ndani ya gari lao.Mgeni huyo wasiyemtarajia alikaa ndani ya gari hilo kwa dakika 10 katika eneo la Gol Kopjes la mbuga hiyo, kabla ya mwishowe kuondoka kwenda kuwinda swara.Britton Hayes anasema walikuwa wamemuangazia duma mmoja aliyekuwa ameruka sehemu ya mbele ya gari lao pale mwingine aliporuka na kuingia kupitia sehemu ya nyuma bila wao kumuona.“Tulianza kugundua duma hao walikuwa wameanza kuvutiwa na gari letu; lakini hatukuwa na muda wa kuondoka au kutoroka kwa sababu hutaki kuwashtua wanyama hao, ukifanya hivyo ndivyo mambo huenda mrama,” Hayes aliambia jarida la Komo News.
“Nilikuwa nimejawa na wasiwasi sana. Lakini wakati wote nilikuwa nauhisi uhai wangu,” anasema.

Hakuna maoni:

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Kurasa