Daraja la kioo China lasitishwa kutumika baada ya - MKWELI BLOG

Karibu kwenye kitovu cha HABARI.

PATA HABARI ZA MICHEZO KUTOKA KILA KONA YA DUNIA NA MAGAZETI KWA WAKATI UKIWA KARIBU NASI

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Jumamosi, 3 Septemba 2016

Daraja la kioo China lasitishwa kutumika baada ya

Daraja la kioo ambalo limeelezwa kuwa liko juu zaidi liliziduliwa hivi karibuni nchini China ambapo lina urefu wa zaidi ya futi 1400, upana wa futi 20 na karibu futi 1000 kutoka kwenye ardhi na imeripotiwa kuwa kioo chake ni imara zaidi mara 25 zaidi ya kioo cha dirisha.

Daraja hilo la wapita kwa miguu lijulikanalo kwa jina la daraja la Zhangjiajie lilizinduliwa August 20 mwaka huu ambapo lina uwezo wa kuchukua watu hadi 800 kwa wakati mmoja. Imeelezwa kuwa daraja hilo limekuwa likitumika kwa shughuli mbalimbali za kiutalii.

Daraja hilo limelazimika kufungwa ili kufanyiwa maboresho ya ndani baada ya idadi kubwa ya watalii waliokusanyika kutembelea kweye daraja hilo. Daraja hilo ambalo liko Kusini mwa China liligharimu dola million 48 kujengwa, na lilifunguliwa August 20 na limesitishwa huduma zake leo.

Msemaji wa kivutio hicho aliiambia MailOnline kuwa daraja lilitengenezwa ili kuweza kuchukua kiwango cha juu cha watu ambao ni 800 kwa wakati mmoja, na limepokea takribani watu 10,000 ambao ni watalii tangu lifunguliwe, msemaji huyo alisisitiza kuwa ni sehemu ya kioo ya daraja ni salama.




pata Habari za kila kona ya dunia hapa

Hakuna maoni:

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Kurasa