Mwana FA Awataja Hawa Ndiyo Wasanii Wake Bora wa Hip Hop Bongo - MKWELI BLOG

Karibu kwenye kitovu cha HABARI.

PATA HABARI ZA MICHEZO KUTOKA KILA KONA YA DUNIA NA MAGAZETI KWA WAKATI UKIWA KARIBU NASI

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Alhamisi, 4 Agosti 2016

Mwana FA Awataja Hawa Ndiyo Wasanii Wake Bora wa Hip Hop Bongo

Mwanamuziki Mwana FA amefunguka na kuwataja wasanii wawili ambao yeye siku zote amekuwa akiwakubali kutokana nauwezo wao na kazi kubwa waliyoifanya katika muziki wa Hip Hop Tanzania kiasi cha kuwafanya watu waamini muziki huo siyo uhuni bali ni kazi.


Mwana FA kupitia kipindi cha Friday Night Live (FNL) kinachorushwa na EATV alisema Professor Jay pamoja na marehemu Albert Mangwea ndiyo wasanii wake wawili bora wa siku zote katika muziki wa Hip hop Tanzania.“Wasanii wangu bora kwa kipindi chote kwenye muziki wa Hip hop ni marehemu Albert Mangwea pamoja na Professor Jay hiyo nasema na kuna siku nilishawahi kuandika hilo, mpka Professor alinipigia simu na kuniuliza mzee una nini unataka kufa nini?. Watu hawajui tu huyu Professor Jay kwanza ndiyo mtu aliyefanya muziki wetu huu kwanza uanze kuheshimiwa, mwanzoni nyimbo zilikuwa na ujumbe wa fujo fujo fulani, kwa hiyo muziki wetu ulikuwa hauchukuliwi ‘serious’ lakini baada yachemsha bongo kila kitu kikabadilika” alisema Mwana FAMbali na hilo Mwana FA alisema kuwa Professor Jay ni msanii ambaye alifanya yeye kidogo aache muziki sababu Mwana FA alikuwa anataka kufanya muziki bora lakini alipokuwa anasikiliza kazi za Professor Jay akaona hawezi kufanya kazi bora kama hizo.“Unajua mimi siku zote huwa nataka kuwa best kwa kile nachofanya sijui kwa wasanii wengine, sasa baada ya kusikia ngoma ya Professor Jay ‘Chemsha bongo’ mimi nina nyimbo zangu nilikuwa nimeandika nikarudi nyuma nakajiuliza sasa mimi nawezaje kuwa ‘best’ kwa ngoma hizi? Yaani alinikatisha tamaa lakini nikarudi na kuanza kujipanga upya” alisema Mwana FA



ni kazi yangu kukujuza

Hakuna maoni:

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Kurasa