Ray C wa Sasa Sio Kama wa Kipindi Kile – Ray C - MKWELI BLOG

Karibu kwenye kitovu cha HABARI.

PATA HABARI ZA MICHEZO KUTOKA KILA KONA YA DUNIA NA MAGAZETI KWA WAKATI UKIWA KARIBU NASI

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Alhamisi, 31 Machi 2016

Ray C wa Sasa Sio Kama wa Kipindi Kile – Ray C

Msanii Ray C amevijia juu vyombo vya habari vianvyoandika taarifa za uongo juu yake, kuwa amerudia kutumia madawa ya kulevya, na kuahidi safari hii atavifikisha mahakamani.


Katika ukurasa wake wa instagrama Ray C ameandika ujumbe mrefu kuhusu vyombo vya habari vinavyomchafua, na kwamba wana mpango wa kukwamisha harakati zake za kupambana na madawa ya kulevya.“Hujuma hizi najua mnazifanya ili niishie njiani katika harakati za kupambana na dawa za kulevya nchini, Mimi na taasis yangu nitaendelea kusonga mbele na hakika sitakwamishwa na nyumbu kama hawa kwanza mwonekano wa picha uko wazi mimi sina nywele fupi kiasi hicho Ray C wa sasa si yule wa kipindi na enzi hizo nowI’m not catalysts of drugs, hata hivyo tayari nimewasiliana na mwanasheria wangu ili niweze kuwawajibisha hawa nyumbu” aliandika Ray C.Pia Ray c amesema kwa sasa yuko kwenye maandalizi ya mwisho kuandaa nyimbo yake, japokuwa bado yuko kwenye dozi ya methadone, inayotibu uathirika wa madawa ya kulevya.“Mimi Niko katika maandalizi yangu ya mwisho ya kuaanda nyimbo yangu japo bado niko katika dose ya methadone”, aliandika Ray c.


Hakuna maoni:

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Kurasa