RAIS MAGUFULI AWATEMA MARC WA JAKAYA KIKWETE 12, YUMO DK RUTENGWE WA MOROGORO. - MKWELI BLOG

Karibu kwenye kitovu cha HABARI.

PATA HABARI ZA MICHEZO KUTOKA KILA KONA YA DUNIA NA MAGAZETI KWA WAKATI UKIWA KARIBU NASI

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Jumatatu, 14 Machi 2016

RAIS MAGUFULI AWATEMA MARC WA JAKAYA KIKWETE 12, YUMO DK RUTENGWE WA MOROGORO.

RAIS Dk. John Magufuli, amefanya uteuzi wa wakuu wa mikoa wapya huku akiwatema 12 wa zamani.Katika uteuzi huo Rais Magufuli ameteuwa majenerali wa wanne wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ)na kuwapangia kazi katika mikoa yamipakani.Taarifa ya Ikulu iliyotolewa jijini Dar es Salaam jana na Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi, Mhandisi Mussa Iyombe ilieeleza kwamba wakuu hao wa mikoa wataapishwa kesho Ikulu.

Katika uteuzi huo wakuu wa mikoa 26 walioteuliwa kati yao 13 ni wapya, saba wamebakizwa katika vituo vyao vya kazi, watano wamehamishwa vituo vya kazi, huku wengine wakipandishwa akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda.Februari 13, mwaka huu Rais Dk. John Magufuli, alilitaja hadharani jina la Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda kuwa mmoja wa watu waliojihakikishia nafasi katika Serikali yake kutokana na utendaji kazi wake.Rais Magufuli aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na wazee wa Dar es Salaam ambapo pamoja na kusifia utendaji kazi wa Makonda, alisema umma usishangae iwapo atampandisha cheo.

Makonda alitajwa kwa kiwango kikubwa kuhamasisha uchangiaji wa elimu na kusimamia shughuli zamaendeleo.

“Najua watu wanauliza sana ni lini nitateua wakuu wa mikoa na wilaya.Wala hawatajua, lakini ninaendelea kuwachambua, angalau mheshimiwa Makonda umeshajihakikishia angalau kupata.Lakini na wewe sasa usianze kulala,”

alisema Rais Magufuli katika mkutano huo na wazee.Kauli hiyo ya Magufuli imeonekana kuwaibua baadhi ya wakuu wa wilaya ambao kwa zaidi ya wiki moja sasa wamekuwa wakisambaza wenyewe au mawakala wao picha za utendaji kazi wao kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii.

Walioteuliwa
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda, ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga (Geita), Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu (Kagera).

Wengine ni Meja Jenerali Mstaafu Raphael Muhuga aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Brigedia Jeneral Mstaafu Emmanuel Maganga (Kigoma) na Godfrey Zambi (Lindi).Wengine ni Dk. Kebwe Steven Kebwe (Morogoro), Kamishna Mstaafu wa Polisi, Zelothe Stephen (Rukwa), Anna Kilango Malecela ( Shinyanga) na Mhandisi Methew Mtigumwe (Singida).

Wengine walioteuliwa ni aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Antony Mataka (Simiyu), aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Aggrey Mwanri (Tabora), huku aliyekuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM na badaye kuwa mshauri wa Rais Jakaya Kikwete wa mambo ya siasa, Martine Shigela akiteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga.

Katika uteuzi huo, Rais Magufuli amewakumbuka na kuwafuta machozi baadhi ya wabunge walioanguka majimboni mwaka jana, ambao walikumbana na upepowa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).Wabunge hao na majimbo yao katika mabano ni Agrey Mwanry (Siha), Anne Kilango (Same Mashariki), Godfrey Zambi (Mbozi Mashariki) na Dk. Kebwe Steven Kebwe (Serengeti).

Waliohamishwa ni aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Jordan Rugimbana kapelekwa Mkoa wa Dodoma, Said Meck Sadick (Kilimanjaro), Magesa Mulongo (Mara), Amos Makalla ( Mbeya) na John Mongella (Mwanza).Waliobaki vituoniRais pia amewateua na kuwabakisha katika vituo vyao vya kazi Amina Masenza (Iringa), Daudi Ntibenda (Arusha),Dk. Joel Bendera (Manyara), Halima Dendegu (Mtwara), Dk. Rehema Nchimbi (Njombe), Evarist Ndikilo (Pwani), Said Mwambungu (Ruvuma) na Luteni Mstaafu Chiku Galawa ambaye amepelekwa Mkoa mpya wa Songwe ulioanzishwa baada ya kugawanywa Mkoa wa Mbeya.

Kiapo
Taarifa hiyo ya Ikulu ilieleza kwamba wakuu wote wa mikoa walioteuliwa wataapishwa kesho saa tatu na nusu asubuhi Ikulu, jijiniDar es salaam.

Waliotemwa
Wakuu wa mikoa waliotemwa na mikoa yao katika mabano ni Dk. Parseko Kone (Singida), Fatma Mwasa (Geita), Ludovick Mwananzila (Tabora), Ally Rufunga (Shinyanga), Eraston Mbwilo (Simiyu), Abas Kandoro (Mbeya), Dk. Rajabu Rutengwe (Morogoro), Mwantumu Mahiza (Tanga).Wengine ni Asery Msangi (Mara) Kanali Mstaafu Issa Machibya (Kigoma), Dk. Ibrahim Msengi (Katavi) na Magalula Said Magalula (Rukwa).

Chekeche kwa Ma-DCPamoja na Rais Magufuli kakamilisha kazi ya uteuzi wa wakuu wa mikoa hivi sasa presha imebaki kwa wakuu wa wilaya, hukutaarifa za ndani zikieleza kwamba wengi wao hawapewi nafasi ya kurejea katika nafasi zao.

Tangu Rais Magufuli alipotangaza Baraza la Mawaziri Desemba mwaka jana, baadhi ya wakuu wa mikoa pamoja na wilaya wameripotiwa kuishi kwa hofu ya kutemwa katika nafasi zao.


Hakuna maoni:

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Kurasa