Waziri wa Magufuli ashitukia majungu - MKWELI BLOG

Karibu kwenye kitovu cha HABARI.

PATA HABARI ZA MICHEZO KUTOKA KILA KONA YA DUNIA NA MAGAZETI KWA WAKATI UKIWA KARIBU NASI

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Jumapili, 21 Februari 2016

Waziri wa Magufuli ashitukia majungu

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji, ametoa onyo kwa watumishi wa Wizara hiyo kuacha kutumia muda mwingi kupiga majungu na badala yake wachape kazi.Waziri Kijaji, alitoa agizo hilo mjini hapa wakati akifungua kikao cha Baraza Kuu la Wafanyakazi wa Taasisi ya Uhasibu (TIA) ambapo aliuagiza uongozi kuendelea kusimamia kwa karibu kazi na kutathiminiutendaji wa watumishi.“Kuna watu kazi yao kupiga majungu huku mezani kwao kumejaa majalada kana kwamba hana kazi ya kufanya,” alisema Dk. Kijaji. “Viongozi wapeni watumishi kazi za kufanya ili nao wapate uzoefu ambao tayari ninyi mmeshapata... waache kupika majungu, tunataka kila mtu atimize wajibu wake vinginevyo watupishe.” Uwajibikaji wa kila mtumishi katika nafasi yake ni muhimu kwa taifa kwani utaletatija katika sehemu ya kazi, alisema na kuwataka watumishi hao kujituma na kufanyakazi kwa bidii kwani wamepewa dhamana ya kuwatumikia Watanzania.Akitoa taarifa ya utendaji kazi wa Taasisi hiyo, Afisa Mtendaji Mkuu wa TIA, Dk. Joseph Kihanda alisema taasisi imejiimarisha katika utoaji wa elimu yenye ubora ili kuwawezesha wahitimu kufanya vizuri katika masomo yao na baadaye katika sehemu zao za kazi.Alisema kuwa jitihada zao za kutoa elimu bora zimethibitishwa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi (NBAA) na bodi ya Wataalam wa manunuzi na ugavi (PSPTB).Hata hivyo, kuna changamoto zinazoikabili taasisi hiyo kwa muda mrefu ikiwamo ya uhaba wa majengo, alisema, kwani kwa miaka minne TIA haijapewa ruzuku kwa ajili ya miradi ya maendeleo.  Changamoto nyingine ni uhaba wa wafanyakazi ambapo uwiano wa wahadhiri haulingani na wanafunzi, alisema Dk. Kihanda.

Hakuna maoni:

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Kurasa