Projecta yakwamisha kesi ya kina Guninita dhidi ya Makobda. - MKWELI BLOG

Karibu kwenye kitovu cha HABARI.

PATA HABARI ZA MICHEZO KUTOKA KILA KONA YA DUNIA NA MAGAZETI KWA WAKATI UKIWA KARIBU NASI

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Jumatano, 3 Februari 2016

Projecta yakwamisha kesi ya kina Guninita dhidi ya Makobda.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imeshindwa kuanza kusikiliza kesi ya  madai iliyofunguliwa na waliokuwa makada wa CCM, Mgana Msindai na John Guninita (kwa sasa ni makada wa Chadema) dhidi ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paulo Makonda,  baada ya kukosekana kwa projekta ya kuonyesha picha zilizorekodiwa siku ya tukio.Wakili wa walalamikiwa Benjamin Mwakagamba alidai mbele ya Hakimu Mkazi Hellen Riwa kwamba, kesi hiyo ilipangwa kuanza kusikilizwa jana ushahidi wa Guninita, lakini ushahidi wake utahusisha kielelezo cha CD lakini kwa kuwa hawakuwa  na projekta aliomba tarehe nyingine ya kusikilizwa.Aidha aliiomba mahakama kuwapatia muda wa siku 14 kwa ajili ya kufanya maandalizi ya kutafuta projekta ya kuonyesha tukio mahakamani.Hakimu Riwa alisema kesi hiyo itaendelea kusikilizwa ushahidi wa Guninita Februari 15, mwakahuu.

Hakuna maoni:

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Kurasa