Dk. Mahiga aanika siri Magufuli kutosafiri nje - MKWELI BLOG

Karibu kwenye kitovu cha HABARI.

PATA HABARI ZA MICHEZO KUTOKA KILA KONA YA DUNIA NA MAGAZETI KWA WAKATI UKIWA KARIBU NASI

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Ijumaa, 5 Februari 2016

Dk. Mahiga aanika siri Magufuli kutosafiri nje

Ataja mambo makuu matatu yanayombakiza Rais nyumbani na kutuma wawakilishi mikutano ya kimataifa�Apotozea pia safari ya Angola�

Zikiwa zimebaki siku sita, Rais John Magufuli, afikishe siku 100 za utawala wake bila kusafiri nje yanchi, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kanda na Kimataifa, Balozi Augustine Mahiga, ameeleza sababu zinazofanya kiongozi huyo kutosafiri nje ya nchi.Akizungumza katika mahojiano maalum na  Nipashe mjini Dodoma jana Balozi Mahiga alisema bado kuna uwezekano Rais Magufuli akaendelea kutosafirikwenda nje ya nchi, akiyataja mambo hayo matatu kuwa ndiyo sababu kuu ya kufanya hivyo.Aliyataja mambo hayo kuwa ni ukata wa fedha alioukuta serikalini wakati akiingia madarakani, kupata muda wa kuendelea kuuda serikali yake na sakata la uchaguzi wa Zanzibar.Kauli hiyo ya Balozi Mahiga ilitokana na swali aliloulizwa na Nipashe juu ya athari ambazo Tanzania inapata kwa Rais Magufuli kutoudhuria mikutano ya kimataifa ukiwamo wa Umoja wa Afrika na ule wa Rais wa China aliyekutana na marais wa Afrika, nchini Afrika Kusini.“Kwa kipindi hiki cha mwanzoni Rais ametoa maelezo, ameomba radhi kwamba yuko kwenye kuunda serikali maana hata kuunda baraza la mawaziri ilichukua karibu mwenzi mzima na hata tunavyozungumza hivi hajakamilisha uunda serikali yake. Mbali na kuunda baraza bado kuna kuteua wakuu wa mikoa, wilaya na wakuu wa taasisi mbalimbali,” alisema na kuongeza:“Lakini pia alikuta serikali iko katika hali ngumu sanakifedha, akaona utendaji kazi lazima asimamie mwenyewe. Kwa hiyo kote huko ambako alitakiwa kwenda kwa miezi sita ya kwanza aliomba radhi na ameeleweka kabisa na ninadhani kazi hii ya kuweka msingi, mwelekeo na msimamo itaendelea kwa mieziminne au mitatu.”Aidha, Balozi Mahiga alisema suala la Zanzibar ambalo hajalimaliza, huku Bunge likiwa ndiyo limeanza vikao vyake ni miongoni mwa mambo yaliyomlazimu Rais Magufuli kukaa nyumbani.Alisema, mbali na kutoaudhuria mikutano hiyo, Rais Magufuli amekuwa akiwahakikisha marais wenzake kwamba baada ya kumaliza hatua za kuunda serikaliyake atakuwa tayari kuonana nao.Alipoulizwa ni vitu gani ambavyo Rais asipovisimamia vinaweza kuharibika, alisema: “Kwa mfano masuala ya usimamizi wa fedha, tumeona taasisi zinavyopambana, watu kupoteza ushahidi, komyuta zinaibiwa, mafaili yanaibiwa, kuna maamuzi mengine ni rais tu anaweza kutoa uamuzi.”“Fikiri unaenda kwenye mkutano unakaa siku tatu huku mambo hayajakamilika, utaona tu bora urudi ukaliweke vizuri, kutengeneza serikali siyo sawa na kupanga timu ya mpira, inachukua muda, kuna kutafuta watu, kuwapima na kuwachuja, tusifikiri serikali ni mawaziri na wakuu wa mikoa tu.”Alisema kuna taasisi muhimu, mashirika ya umma yapo mengi na yanahitaji mabadiliko, hivyo Rais ni lazima asimamie. “Kwakweli Rais wetu ana nguvu yakipekee, kwa sababu kwa siku labda ana saa tatu tu za usingizi,” aliongeza kusema.FEDHA ZILIZOOKOLEWABalozi Mahiga alisema hana takwimu za moja kwa moja za juu ya fedha zilizookolewa kwa Rais kutosafiri nje, ingawa ana amini gharama zimepungua kwa kiasi kikubwa.“Naweza kusema tumepunguza sana matumizi ya safari na tumetenga kati ya safari za Rais na zile za wizara kwa sababu huko nyuma safari za Rais na watu wake viongozi wakubwa zote zilikuwa zinajumuishwa kwenye gharama za safari za wizara ndiyo maana zilikuwa zikionekana ni kubwa,” aliema.Alisema pamoja na kwamba Rais hajaanza kusafiri nje ya nchi, lakini ametoa maagizo ambayo yameanza kutekelezwa, ikiwamo balozi zimeanza kupewa uwezo wa ziada kama wataalamu wanaofaa,watumizshi wa kutosha na kupatiwa fedha za kukidhimahitaji katika kuwakilisha nchi na hasa katika kushirikiana na kampuni, mashirika na kanda.“Agosti kuna mkutano wa Organ of Peace and Security wa Sadc ambao Tanzania itakuwa mwenyekiti, hii lazima Rais awepo, mwenyekiti wake lazima daima awe Rais, lakini siyo lazima aende Gaborone anaweza kuita wenzake hapa.”“Rais mwenyewe ameeleza kwamba anapunguza matumizi, kwa hiyo yawezekana kabisa kwenye mkutano wa siku tatu anaweza kwenda kwa siku moja na nusu, au badala ya kwenda na wasaidizi 30 ataenda na 15, juzi tulivyokwenda na Makamu wa Rais Addisababa, Ethiopia, awali kwenye safari kamaile watu 30 mpaka  35 ndio walikuwa wakienda, lakini juzi alikuwa na watu 15, mimi kwa wizara yangu walikuwa wawili na wengine wote walionisaidia walitoka kulekulekule,” alisema.

Hakuna maoni:

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Kurasa