W atu sita wanaodaiwa kuwa majangili, wanashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kuitungua helikopta ya doria na kusababisha kifo cha rubani wake katika pori la akiba la Maswa.Kukamatwa kwa watu hao kumekuja siku moja baada ya Rais, John Magufuli, kutoa agizo kwa Wizara ya Maliasili na Utalii kuwakamatwa waliohusika na tukio hilo na kufikishwa katika mkonoya sheria.Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Gerson Msigwa, akizungumza na Nipashe jana alisema Rais Magufuli mbali na kusikitishwa na tukio hilo, pia aliuakikisha umma kuwa serikali itahakikisha inaendeleza mapambano dhidi ya ujangili kwa nguvuzote na kuwataka wananchi na wadau mbalimbali wa hifadhi ya wanyamapori kutokatishwa tama.Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Simiyu, Gemini Mushy, jana alithibitisha kwa njia ya simu kukamatwa kwa watu hao.Alisema watuhumiwa hao walikamatwa juzi na wanalisaidia jeshi hilo katika uchunguzi wake kufuatia tukio hilo.Ijumaa iliyopita, watu wasiojulikana, waliitungua helikopta hiyo wakati ikifanya doria katika pori hilo baada ya kuwapo taarifa kwamba majangili walikuwa wameua tembo mmoja.Katika tukio hilo, rubani wa helikopta hiyo raia wa Uingereza, Rodgers Gower (37) alikufa, huku mwenzake Nicky Bester wa Afrika Kusini akinusurika.
Post Top Ad
Responsive Ads Here
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Post Bottom Ad
Responsive Ads Here
Author Details
Templatesyard is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates which are professionally designed and perfectlly seo optimized to deliver best result for your blog.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni