Kinadharia, Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara ambayoleo inaingia katika duru la pili ni shindano linaloendeshwa kwa mujibu wa kanuni zilizotungwa, na zinazosimamiwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).Kwamba kabla ya ligi ya Bara kuanza panakuwa na jopo au kamati ya ligi inayoandaa ratiba kwa kuzingatia kalenda ya matukio ya soka la kitaifa na kimataifa na mechi za ligi yenyewe zinaendesha kwamisingi ya kikanuni na Sheria 17 za Soka.Kinyume cha matarajio ya wengi, watendaji wakuu wa shirikisho ndiyo wanaongoza kwa kuweka kando kanuni na taratibu za uendeshaji wa ligi hiyo kiasi cha kuibua mvutano na timu shiriki.Baada ya kumalizika kwa mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo msimu huu, TFF ilisahau kwamba msimu uliopita ililalamikiwa mno na wadau kuhusu panguapangua ovyo kwa ratiba ya ligi, iliiruhusu Azam FC kwenda Zambia kushiriki mashindano ya 'ndondo' ya timu nne.Kuondoka kwa Azam FC kumeathiri mtitiriko mzima wa ratiba ya ligi hiyo kwani sasa kamati ya uendeshaji wa ligi italazimika kupanga tarehe mpya kwa ajili ya mechi mbili za timu hiyo ya Chamazi dhidi ya Tanzania Prisons na Stand United.Itakumbukwa kuwa mwaka jana Nipashe tulieleza kuwa 'utitiri' wa mechi za viporo ni miongoni mwa mbinu chafu zinazotumika kupanga matokeo ya mechi za ligi hiyo. Na TFF wanalitambua hilo, ndiyo maana wakaahidi msimu uliopita kwamba wasingerudia makosa hayo.Kwa kuzingatia athari za kadhia ya upangaji matokeo kwa soka la Tanzania na maendeleo ya taifa, Nipashe hatukutarajia kuona watendaji wakuu wa shirikisho wakiweka pamba masikioni na kuiruhusu Azam kukacha ratiba ya ligi ya Bara na kutimkia Zambia.Hivi karibuni, Bodi ya Ligi Kuu (TPLB) ilieleza kuwa idadi ya watu wanaoingia viwanjani kutazama mechiza ligi hiyo imekuwa ikipungua, moja ya sababu ikitajwa kuwa matangazo ya moja kwa moja ya televisheni ya mechi za ligi hiyo.Lakini Nipashe tunaona kitendo cha TFF kukiuka mara kwa mara misingi ya weledi katika uendeshaji wa ligi hiyo ndiyo sababu kuntu ya kupungua kwa watazamaji viwanjani.Ndiyo maana, tunasisitiza TFF inapaswa kurejea katika misingi ya weledi kuhakikisha ligi ya Bara inaendeshwa kwa haki kwa timu zote 16 zinazoshiriki. Tunaamini ni udhalilishaji kupangua ratiba ya Ligi Kuu kupisha mechi za 'ndondo' ambazo hazimo hata kwenye kalenda ya matukio ya soka.Uzembe huu, tunasema Nipashe, unaweza kuonekana kitu cha kawaida kwa uongozi wa sasa TFF, lakini athari yake ni kubwa katika kuharibu na kudidimiza soka la Tanzania.Tunaamini kuyumba na kupungua kwa mvuto wa ligihiyo kutakimbiza wadhamini ambao walikuwa wameaanza kumininika kwa wingi kuipa nguvu TFF kiuendeshaji.Shime, TFF inapaswa kurejea kwenye misingi ya weledi na kutumia nasaha za Hayati Mwl. Julius Nyerere kwa KUJISAHIHISHA kuhakikisha kunakuwa na heshima ya ligi kuu ya Bara.
Post Top Ad
Responsive Ads Here
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Post Bottom Ad
Responsive Ads Here
Author Details
Templatesyard is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates which are professionally designed and perfectlly seo optimized to deliver best result for your blog.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni