Shahidi augua ghafla, kesi yaahirishwa - MKWELI BLOG

Karibu kwenye kitovu cha HABARI.

PATA HABARI ZA MICHEZO KUTOKA KILA KONA YA DUNIA NA MAGAZETI KWA WAKATI UKIWA KARIBU NASI

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Jumamosi, 23 Januari 2016

Shahidi augua ghafla, kesi yaahirishwa

Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Moshi imelazimika kuahirisha kwa siku mbili mfululizo, kesiya mauaji ya mfanyabiashara, bilionea wa madini ya tanzanite, Erasto Msuya (43), baada ya shahidi wa tisa, Inspekta Samuel Maimu (45), kutoka Ofisi ya Mkuu wa Upepelezi wa Mkoa wa Kilimanjaro (RCO), kuugua ghafla wakati akitoa ushahidi.Shahidi huyo, aliyeanza kutoa ushahidi wake juzi, aliugua ghafla jana na kupelekwa katika Hospitali ya Rufani ya Mkoa wa Kilimanjaro (Mawenzi) kwa ajili ya kupatiwa matibabu.Msuya aliuawa kwa kupigwa risasi, Agosti 7, mwaka 2013, saa 6:30 mchana katika eneo la Mijohoroni, kando kando ya Barabara Kuu ya Arusha-Moshi, karibu na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).Kabla ya kuahirishwa kwa kesi hiyo ya mauaji ya kukusudia, Wakili Mkuu wa Serikali, Neema Mwanda,akiwa mbele ya Jaji Salma Maghimbi anayesikiliza shauri hilo, alidai kuwa kesi hiyo ilikuwa iendelee jana kwa ajili ya kusikiliza ushahidi kutoka kwa shahidi wa tisa wa upande wa mashtaka ambaye hakumaliza kutoa ushahidi kutokana na kuugua ghafla juzi wakati akitoa ushahidi wake.Wakili Neema alidai: “Mheshimiwa Jaji, kwa bahati mbaya shahidi wetu (Inspekta Samuel), jana (juzi) alipata tatizo la kiafya akiwa anatoa ushahidi wake mahakamani na alienda kupatiwa matibabu Hospitali ya Mawenzi na kwa taarifa tulizo nazo, bado anaendelea na matibabu.“Tumeshindwa kupata taarifa ya daktari na leo (jana), alikuwa achukuliwe vipimo. Kwa maana hiyo upande wa mashtaka tunaomba kesi hii iahirishwe hadi Jumatatu ijayo ili tuweze kufuatilia afya yake natuwasilishe mahakamani taarifa ya daktari, kuhusu uchunguzi wa afya yake na matibabu aliyopata.Baada ya Neema kutoa hoja hiyo, Jaji Salma alilihoji jopo la mawakili wa upande wa utetezi iwapo wana pingamizi kuhusu hoja ya kuahirishwa kwa kesi hiyo.Kiongozi wa jopo hilo, Wakili John Lundu, alisimama na kuieleza mahakama kwamba kutokana na sababuzilizotolewa, hawana  pingamizi na wako tayari kuahirishwa kwa kesi hiyo.Kutokana na pande zote kuafikiana, Jaji Salma alisema mahakama hiyo imejiridhisha baada ya kupima hoja iliyotolewa na upande wa mashtaka, na kisha kuafikiwa na jopo la mawakili wa utetezi, na hivyo imeamua kuahirisha kesi hiyo hadi Jumatatu ijayo.Washtakiwa wanaokabiliwa na kesi hiyo ni Sharif Athuman (31), ambaye ni mfanyabiashara wa madinina mchimbaji mdogo, mkazi wa Kimandolu mkoani Arusha, Shaibu Saidi maarufu kama “Mredii” (38), mkazi wa Songambele, Simanjiro mkoani Manyara na Mussa Mangu (30).Wengine ni Jalila Said (28), mkazi wa Babati mkoani Manyara, Sadiki Jabir a.k.a “Msudani” (32), mkazi wa Dar es Salaam na Lang’ata, wilaya ya Hai, Karim Kihundwa (33), mkazi wa Lawate, wilaya ya Siha na Alli Musa maarufu “Mjeshi”, mkazi wa Babati.Katika ushahidi wake alioutoa mahakamani hapo juzi, Inspekta Maimu  alidai kuwa Agosti 7, 2013 majira ya saa sita mchana, akiwa ofisini alipigiwa simu ya mkononi na RCO (Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa) wa Kilimanjaro, akimweleza kwamba kuna mauaji yametokea huko maeneo ya Bomang’ombe, kwa hiyo achuke timu ya Seene of Crime na CRT (Crisis Response Team) na waende huko.Shahidi huyo alidai baada ya kufika eneo la mauaji, alimtambua Msuya baada ya kufanya ukaguzi na kukuta karatasi yenye jina lake ikiwa ndani ya gari lake aina ya Range Rover, rangi ya kijivu lenye namba za usajili T 800 CKF.Alidai kuwa alilazimika kulipekua gari hilo na kukuta bastola moja,   simu mbili za Samsung na Iphone zikiwa ndani ya gari hilo, huku gari hilo likiwa na namba ya utengenezaji (Chasses number), SALG A2HE 90A104163.Aidha, shahidi huyo alidai kuwa katika eneo la tukio la mauaji ya mfanyabiashra huyo wa madini, waliokota maganda 22 ya risasi na kuukuta mwili wamarehemu ukiwa na matundu ya risasi katika mwili wake.Aliendelea kudai kuwa kabla ya kuuchukua mwili wa marehemu na kwenda kuuhifadhi katika Hospitali ya Wilaya ya Hai (Bomang’ombe), alichora ramani ya eneo la tukio.“Tukiwa bado eneo la tukio tulipata taarifa kwamba kuna pikipiki aina ya Toyo imeonekana imetelekezwaupande wa kaskazini mwa tukio la mauaji (kijiji cha Orkolili) ikiwa pamoja na Helmet (kofia ngumu) na jaketi moja,” alidai shahidi huyo wa tisa.Ifuatayo ni sehemu ya ushahidi alioutoa kama alivyohojiwa na Wakili Mwandamizi wa Serikali, Abdalah Chavula;Wakili:  Mtu uliyemkuta amefariki katika eneo la tukioulikuwa unamfahamu?Shahidi: Hapana, nilikuwa simfahamu.Wakili: Umezungumzia habari za uchoraji wa ramani,nani alichora katika tukio la kwanza?Shahidi: Nilichora mimi.Wakili: Ramani hiyo ukionyeshwa siku ya leo unaweza kuitambua?Shahidi: Ndiyo, naweza kuitambua.Wakili: Ni kitu gani kitakufanya utambue ramani hiyo?Shahidi: Nitaitambua kwa sababu ina mwandiko wangu, niliandika jina langu na niliweka saini yangu.Wakili: Je ungependa ramani hiyo itolewe kama kielelezo mahakamani hapa?Shahidi: Ndiyo, ningependa itolewe kama kielelezo mahakamani hapa.Hata hivyo, mahakama hiyo ilikubali kupokea ramaniya eneo ambalo linadaiwa kufanyika mauaji ya mfanyabiashara, bilionea wa madini ya tanzanite, Erasto Msuya.Jaji Salma alipokea kielelezo hicho, hivyo kumaliza ‘utata’ wa mvutano wa kisheria kuhusu hoja za mawakili wa utetezi, kupinga kupokewa mahakamanikwa kielelezo hicho.Jopo la mawakili wa utetezi katika kesi hiyo linaongozwa na Hudson Ndusyepo, anayemtetea mshitakiwa wa kwanza, Majura Magafu anayemteteamshitakiwa wa pili na wa tano, Emmanuel Safari anayemtetea mshitakiwa wa tatu na John Lundu anayemtetea mshitakiwa wa tano, sita na saba.Katika kesi hiyo, pia upande wa mashtaka unaongozwa na Wakili Mkuu wa Serikali, Neema Mwanda akisaidiwa na Wakili Mwandamizi wa serikali Abdala Chavula, Wakili Mwandamizi Stella Majaliwa na Baraka Nyambita.Hadi sasa jumla ya mashahidi wanane wa upande wa mashtaka, wameshatoa ushahidi wao mahakamani hapo akiwamo aliyekuwa Mkuu wa Upepelezi (OC-CID) wa Wilaya ya Hai, Joash Yohana, Mganga Mkuu wa Wilaya (DMO) ya Hai, Dk. Paul Chaote (39) na Khalid Sankamula (49) ambaye ni Mganga wa Kienyeji na Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Limbula, Kaliua mkoani Tabora.

Hakuna maoni:

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Kurasa