Bunge lashauriwa kurejesha POAC. - MKWELI BLOG

Karibu kwenye kitovu cha HABARI.

PATA HABARI ZA MICHEZO KUTOKA KILA KONA YA DUNIA NA MAGAZETI KWA WAKATI UKIWA KARIBU NASI

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Jumamosi, 23 Januari 2016

Bunge lashauriwa kurejesha POAC.

Shirika lisilo la kiserikali la Sikika, limeshauri kurejeshwa kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge iliyokuwa inashughulikia Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC).Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana na Mkurugenzi Mtendaji wa Sikika, Irenei Kiria, imeeleza umuhimu wa kamati hiyo ambayo moja ya kazi zake ilikuwa ni kutathmini ufanisi wake, kufuatilia utekelezaji wa sera ya ubinafsishaji wa mashirika hayo na kuainisha maeneo sugu ya matumizi mabaya ya fedha za umma.“POAC ilianzishwa mwaka 2008, ilivunjwa na Bunge mwaka 2012 baada ya kufanya kazi kwa ufanisi kwa takribani miaka mitano.Sababu za kuvunjwa POAC zilielezwa kuwa ni kuunganisha wizara na taasisi zake ili ziwe na msemaji mmoja,” alisema.Kiria alisema ripoti za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), zimekuwa zikionesha matumizi mabaya ya rasilimali za umma kuanzia serikali kuu, halmashauri, na kwenye baadhi ya mashirika ya umma.Mkurugenzi huyo alisema Bunge lililopita lilifanyia kazi mambo machache yaliyoibuliwa na CAG, baadhikiasi, lakini mengi hayakufanyiwa kazi kabisa, na CAG alieleza mara nyingi katika ripoti zake kwamba serikali haifanyii kazi mapendekezo yake yote kabla ya ukaguzi unaofuata.Alisema pamoja na upungufu huo, Bunge liliunganisha majukumu ya iliyokuwa POAC kwenye Kamati ya Hesabu za Serikali Kuu (PAC) na kubadili sheria ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali ya 2008 kuruhusu Bunge lisijadili ripoti za CAG hadi  serikali itakapojibu hoja za CAG zilizopo kwenye ripoti hizo.Alisema kwa kipindi hiki kamati hiyo ingekuwa muhimu kwa kuwa CAG anakaribia kukamilisha ripoti ya ukaguzi wa mashirika takribani 180, wizara na idara za serikali kuu sitini, sekretariati za mikoa 25, ofisi za balozi 34, wakala wa serikali 25, mifuko maalum 12 na taasisi nyinginezo za serikali kuu na ripoti zote zifanyiwe kazi na Bunge kupitia kamati zake.

Hakuna maoni:

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Kurasa