Mwili wa Leticia kuwasili nchini kabla ya Jumatatu - MKWELI BLOG

Karibu kwenye kitovu cha HABARI.

PATA HABARI ZA MICHEZO KUTOKA KILA KONA YA DUNIA NA MAGAZETI KWA WAKATI UKIWA KARIBU NASI

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Alhamisi, 14 Januari 2016

Mwili wa Leticia kuwasili nchini kabla ya Jumatatu

Kuna uwezekano mwili wa aliyekuwa Mbunge wa VitiMaalum (Chadema), Leticia Nyerere, aliyefia nchini Marekani utawasili nchini mapema kwa ajili ya maziko tofauti na ratiba iliyokuwa imepangwa awali.Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Msemaji wa familia ya Mwalimu Nyerere, Rose-Mary Nyerere, alisema Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Wilson Masilingi, kwa kushirikiana na familia hiyo wanafanya jitiahada kuusafrisha  mwili huo kuja nchini kabla ya Jumatatuiliyokuwa imepangwa awali.“Ratiba inaonyesha mwili utawasili nchini Januari 18kulingana na taratibu za safari, ila tunajaribu kuangalia njia ya kufupisha muda huo kwa sababu nimbali tangu mpendwa wetu Leticia alipotutoka,” aliasema.Alisema mwili huo baada ya kuwasili nchini utaagwa nyumbani kwa Mwalimu  Nyerere, Msasani, jijini Dar es Salaam na taratibu za kuusafirisha kwenda kijijini Butiama, mkoani Mara kwa ajili ya maziko zitaendelea.Miongoni mwa viongozi wa serikali waliofika jana nakutoa rambirambi kwa familia ya Nyerere ni Spika wa Bunge, Job Ndugai.Leticia alifariki dunia katika Hospitali ya Doctors Community iliyopo Lan ham, Maryland, nchini Marekani na msiba nchini humo upo DMV 9004 Brightlea Court, Lanham, MD 20706.Marehemu ameacha watoto watatu, wawili wa kike na mmoja wa kiume.

Hakuna maoni:

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Kurasa