Mwigulu: Wezi wote wa fedha za wakulima wapandishwe kizimbani. - MKWELI BLOG

Karibu kwenye kitovu cha HABARI.

PATA HABARI ZA MICHEZO KUTOKA KILA KONA YA DUNIA NA MAGAZETI KWA WAKATI UKIWA KARIBU NASI

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Alhamisi, 28 Januari 2016

Mwigulu: Wezi wote wa fedha za wakulima wapandishwe kizimbani.

Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mwigulu Nchemba, amewaagiza viongozi kuhakikisha wale wote waliohusika na wizi wa fedha za wakulima kufikishwa mahakamani mara moja.Alitoa agizo hilo bungeni jana wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe, aliyehoji kuhusiana na ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ya mwaka 2013 iliyoelezea upotevu wa Sh. bilioni 28 za wakulima wazao la tumbaku mkoani Tabora.Nchemba alisema hiyo ripoti anaifahamu na kuagiza wale wote waliohusika katika kuwaibia wakulima hao kuchukuliwa hatua.Alisema suala hilo halipo kwenye tumbaku tu, kwani kuna maeneo mengine ambayo yana changamoto hiyo ya wakulima kuibiwa fedha zao na kuahidi kuwashughulikia wote waliohusika baada ya Bunge kumalizika.Alisema serikali imepanga kupitia makato yote yanayokatwa kwa wakulima na ndani ya siku mbili atatoa tamko juu ya suala hilo.Nchemba alisema Rais John Magufuli ameshaonyesha kukerwa na tozo nyingi za makato kwa wakulima, hali ambayo inawafanya wakose maendeleo, hivyo atalishughulikia suala hilo kwa wakati.

Hakuna maoni:

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Kurasa