Mbunge wa Jimbo la Mlalo wilayani Lushoto Mkoani Tanga (CCM) Rashid Shangazi amesema ataishauri serikali kufungua mpaka wa Tanzania na Kenya uliyopo Kivingo Kata ya Lunguza Wilayani Lushoto kwa lengo la kuwawezesha wakulima Jimbo hilo kuuza mazao yao nchi hiyo ya jirani.Shangazi aliiambia NIPASHE kuwa suala la kero ya soko kwa wakulima wa Kata ya Lunguza ni kubwa na kwamba mazao ya kilimo ikiwemo mbogamboga yamekuwa tatizo kwa wakulima kuuza nchini Kenya ambapo kuna soko la uhakika.Alisema kwa serikali kufungua mipaka hiyo ndio itakuwa njia pekee ya kuweza kuwapa soko la uhakika wakulima wa kilimo cha mbogamboga na mazao mengine Jimboni humo ili waweze kunufaika nacho kuliko ilivyokuwa sasa.Hata hivyo Shangazi alibainisha kuwa sambamba nahilo kazi nyingine atakayoshughulikia ni ukarabati wa barabara ya kutoka Kata ya Mtae hadi Mnazi ambayo itaanza kwa njia ya changarawe ili kuhakikisha miundombinu inaimarika na kuweza kupitika nyakati zote.“Naahidi kuhamasisha utalii kwenye Jimbo hilo kwa kutafutawawekezaji watakaoweza kujenga mahotel kutokana na Jimbo hilo kupakana na misitu ya asili na Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi ambayo itasaidia kutoa ajira kwa wananchi na kukuza pato lao na jamii kwa ujumla “alisema Shangazi.Aidha pamoja na hayo aliwataka wananchi wa jimbo hilo kuhakikisha wanashirikiana bega kwa bega ili kusukuma kasi ya maendeleo yao kwa kuzipatia ufumbuzi changamoto mbalimbali ambazo zinawakabili.Akizungumzia namna atakavyoweza kukabiliana na changamoto zilizopo kwenye sekta ya Afya, Shangazi alisema atahakikisha anaongeza majengo ya vituo vya afya ili kuweza kuzipatia ufumbuzi changamoto zilizopo za uchache wake.Hata hivyo alisema mipango yake kwa vijana ni kuhakikisha kila kijiji kinapewa shilingi milioni 50 kupitia waratibu kata ili kuunda vikundi vya wajasiriamali 10-30 ili waweze kujiendeleza sambamba na kujikwamua kupitia uchumi wao.
Post Top Ad
Responsive Ads Here
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Post Bottom Ad
Responsive Ads Here
Author Details
Templatesyard is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates which are professionally designed and perfectlly seo optimized to deliver best result for your blog.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni