Zaidi ya Sh. Bilioni 6.1 zitagharamia ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami katika halmashauri ya Manispaa ya Singida, zenye urefu wa kilomita 1.8 kwa kipindi cha mwaka wa fedha wa 2015/16.Gharama ya fedha hizo zitatokana na ufadhili wa benki ya dunia, yenye lengo la kuboresha miundombinu ya barabara za mji wa Singida, ikiwemo ile inayoanzia stendi ya zamani hadi kituo kikuu kipya cha mabasi, kilichopo eneo la Misuna yenye urefu wa kilomita 1.8.Mhandisi wa ujenzi wa katika Manispaa hiyo, Lambert Bayona, alisema kuwa ujenzi wa barabara hiyo unatekelezwa na kampuni ya Hari Singh and Sons LTD, kutoka Moshi mkoani Kilimanjaro na itakamilika desemba mwaka huu.Hata hivyo mhandisi huyo alifafanua kuwa, mradi huo wa barabara utahusisha pia na ujenzi wa njia ya waendao kwa miguu na uwekaji wa taa za barabarani.Aidha Bayona alifafanua kuwa, mradi huo utahusisha pia ujenzi wa kituo cha mabasi madogo katika eneo la Majengo, karibu na kituo kikuu cha mabasi cha zamani.“Licha ya ujenzi wa barabara, mradi huu utahusisha pia ujenzi wa kituo kikuu kipya cha mabasi ya mikoani kilichoko Misuna…nacho kitakarabatiwa na kujengwa kwa utaalamu wa hali ya juuu ikiwemo kuwekewa matofali maalumu madogo, ili kukidhi ubora,"alisema mhandisi huyo.Alisema kuwa, baada ya kukamilika kwa awamu ya kwanza, hatimaye ujenzi wa barabara nyingine ya urefu wa kilometa 12 zinatarajiwa kujengwa kwa kiwango cha lami, lakini akafafanua kuwa utekelezajiwake utaanza baada ya kupatikana kwa fedha.Bayona alizitaja baadhi ya barabara hizo kuwa ni ile inayoanzia katika eneo la Peoples hadi kwenye maghala ya national milling, pia barabara inayoanziaofisi za TRA hadi kwa askofu Mabula.Akizungumzia utekelezaji wa mradi huo, Mkurugenzi wa Manispaa ya Singida, Joseph Mchina alisema kuwa, ujenzi huo ni mwendelezo na juhudi katika kuboresha mji wa Singida, ili miundo mbinu ya barabara iweze kupitika kwa urahisi zaidi na kituo cha mabasi kuwa cha kisasa.
Post Top Ad
Responsive Ads Here
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Post Bottom Ad
Responsive Ads Here
Author Details
Templatesyard is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates which are professionally designed and perfectlly seo optimized to deliver best result for your blog.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni