Rais, John Magufuli amewatunuku kamisheni kwa cheo cha Luteni Usu, maoafisa wanafunzi wapya 205pamoja na kutoa nishani kwa maafisa watano waliofanya vizuri kwenye masomo yao.Rais alitoa Kamisheni hiyo kwa cheo cha Luteni Usu jana katika Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli (TMA) ikiwa ni mara yake ya kwanza tangu aingie madarakani.Miongoni mwa maofisa watano hao waliofanya vizuri, wawili ni wanawake ambao ni Efrasia Bundalakutoka Tanzania na Winnie Indumuli kutoka Kenya.Wanaume hao ni Phinias Kiganga aliyefanya vyema darasani, Frank Kitalekwa aliyefanya vyema upande wa medani na Ahmed Mmang'anda aliyefanya vyema darasani pia.Katika jumla ya Luteni Usu 205, wanawake ni 16.Aidha, miongoni mwa wahitimu hao wawili wanatokanchini Burundi, wanne Kenya na wengine wanne Uganda, ambazo ni nchi rafiki.Mara baada ya kutoa kamisheni kwa maofisa hao, Rais Magufuli alipata burudani kutoka kwaya ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kambi ya Oljoro, ambayo nyimbo zake zilimpongeza Rais kwa utendaji wake wa kazi na kumuomba kuendelea na kasi yake ya kusafisha serikali.Nayo bendi ya Jeshi la Watanzania (JWTZ) iitwayo Chacharika ilikonga nyoyo za wananchi waliofurika kushuhudia ndugu zao waliotunukiwa kamisheni huku wakimpongeza kwa utoaji wa elimu bure.Awali, akiingia uwanjani kwa ajili ya ukaguzi wa gwaride, Rais Magufuli alishangiliwa kwa nguvu na wananchi mbalimbali waliohudhuria sherehe hizo wakiwemo viongozi wa serikali pamoja na wageni waalikwa.
Post Top Ad
Responsive Ads Here
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Post Bottom Ad
Responsive Ads Here
Author Details
Templatesyard is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates which are professionally designed and perfectlly seo optimized to deliver best result for your blog.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni