Kwa ufupi*.Lilijengwa pamoja na lile lililoanguka na kuua watu 37 katika Mtaa wa Indira Gandhi*.Jengo hili la ghorofa 16, lililopo mtaa wa Indira Gandhi jijini Dar es Salaam, liliamriwa kubomolewa baada ya kubainika lilijengwa chini ya kiwango.Hatua hiyo ilitokana na jengo pachala ghorofa hiyo kuporomoka Machi 29 mwaka 2013 na kusababisha vifo vya watu 37 na wengine 18 kujeruhiwa. MwananchiDar es Salaam.Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi ametoa siku 18 kwa uongozi wa Manispaa ya Ilala kuvunja jengo la ghorofa 16 lililopo katika Mtaa wa Indira Gandhi kabla halijaleta maafa.Akizungumza jana katika jengo hilo, Lukuvi alisema anashangaa hadi sasakazi ya kuvunja jengo hilo haijaanza licha ya manispaa kuelekezwa kulivunja.Uamuzi wa Serikali kulivunja ulikuja baada kuporomoka kwa jengo katika mtaa huo lililosababisha vifo vya watu37 na wengine 18 kujeruhiwa mwaka 2013.“Ni aibu, manispaa mnataka jengo hiloliporomoke na kuua watu tena! Tutachekwa kwa uzembe kama ikitokea tena ajali,” alisema.Lukuvi alisema kuanzia Februari Mosi uvunjaji wa jengo hilo unatakiwa kuanza vinginevyo wahusika wajiandae kuchukuliwa hatua.“Nataka nikipita hapa siku yoyote kuanzia mwezi ujao nikute mkandarasi anabomoa jengo hili vinginevyo hatutaelewana,” alisema.“Hili ni eneo hatarishi hata tuliosimama hapa hatari yoyote inaweza kutukuta lakini Manispaa ya Ilala haioni kwamba hapa kuna tatizo,”alisema.Waziri alisema uvunjaji wa jengo hilo utakapoanza, wananchi wanaoishi jirani watatakiwa kuhama kwa muda kwa tahadhari.“Mkuu wa Wilaya ya Ilala, wakianza kuvunja jengo hilo tafadhali waondoeni wakazi wote kwa sababu eneo hili litakuwa hatarishi,” alisema.Jengo hilo linamilikiwa kwa pamoja kati ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) na Ali Raza Investment.Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Isaya Mngulumi alisema kilichochelewesha ni makandarasi walioshinda zabuni hiyo kujitoa katika hatua za mwisho wakitoa sababu mbalimbali.Alisema hivi sasa amepatikana mkandarasi Patty Interplan ambaye yuko katika hatua za mwisho za kupewa kazi hiyo.“Tutaanza kazi kama ulivyoelekeza,” alisema Mngulumi.Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi, alisema atatoa ushirikiano kwamanispaa hiyo ili kuhakikisha jengo hilo linabomolewa.
Post Top Ad
Responsive Ads Here
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Post Bottom Ad
Responsive Ads Here
Author Details
Templatesyard is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates which are professionally designed and perfectlly seo optimized to deliver best result for your blog.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni