Askari polisi auawa akifanya ujambazi - MKWELI BLOG

Karibu kwenye kitovu cha HABARI.

PATA HABARI ZA MICHEZO KUTOKA KILA KONA YA DUNIA NA MAGAZETI KWA WAKATI UKIWA KARIBU NASI

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Ijumaa, 29 Januari 2016

Askari polisi auawa akifanya ujambazi

Askari  polisi  Konstebo Norbert Chacha (25) ameuwawa kwa kupigwa risasi kifuani na mgongoni wakati akifanya ujambazi.Mauaji ya askari  huyo yalitokea usiku wa kuamkia juzi usiku wa manane katika kijiji cha  Ibindi, wilayaniMlele, akiwa na watu wengine ambao walikuwa wamekwenda kufanya ujambazi kwenye nyumba ya mfanyabiashara wa madini ya dhahabu kijijini hapo.Diwani wa Kata ya Machimboni, Raphael Kalinga, aliwaambia waandishi wa habari kuwa  askari huyo akiwa na kundi la majambazi wenzake, ambao idadi yao haikufahamika, walifika kijijini hapo kwa lengo lakumvumia na kumpora mfanyabiashara huyo, DanielJohn.Alisema baada ya kufika nyumbani kwa mfanyabiashara huyo, walivunja mlango wa mbele, wakati mfanyabiashara huyo akiwa amelala.Majambazi hayo, alisema baada ya kuvunja mlango, waliingia ndani  na  mfanyabiashara aliwauliza ni kinanani na ndipo walipomwamuru  asipige kelele vinginevyo watamuua.Kalinga ambaye ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo,  alisema kutokana na amri hiyo, John alichukua bunduki yake ya shotgun na kufyatuarisasi ambayo ilimpiga askari huyo kifuani na mgongoni na kufa hapo hapo.Alisema majambazi wenzake ambao walikuwa na  mapanga  na shoka baada ya kuona mwenzao kapigwa risasi na kufa waliamua kumbeba marehemu na kwenda kumtupa kichani umbali wa mita 200 kutoka kwenye eneo la tukio na kisha walitokomea kusiko julikana.Wakazi wa Kijiji hicho walifika nyumbani kwa mfanyabiashara  huyo na kukuta michirizi ya damu na ndipo walipoamua kuifuata ilikokuwa inaelekea.Alisema wanakijiji waliendelea kuifuata michirizi hiyona  walipofika umbali wa mita 200 kutoka nyumbani kwa  John,  waliuona  mwili  wa askari polisi huyo ambaye alikuwa  amefariki dunia kutoa taarifa polisi wilaya ya Mpanda.Polisi walifika kwenye eneo hilo baada ya muda  mfupi na  ndipo walipomtambua marehemu  kuwa ni askari polisi wa kituo cha  cha wilaya ya Mpanda .Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi, Dhahiri Kidavashari, amethibitisha kuuwawa kwa askari huyo kuwa alipigwa risasi  akiwa katika harakati za kufanya ujambazi na kupora .Alisema mwili wa marehemu bado umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti katika Hospitali ya Wilaya ya Mpanda .Kabla ya tukio hilo, kulikuwa na malalamiko kutoka kwa wananchi wa mkoa wa Katavi waliokuwa wakiwatuhumu baadhi ya askari polisi kuhusika katika matukio  ya ujambazi na uporaji mkoani hapa

Hakuna maoni:

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Kurasa