Hivi karibuni msanii wa Bongo
Fleva Amini aliagwa rasmi na nyumba ya kukuza vipaji THT ambako
alikuwepoo kwa zaidi ya miaka 10 tangu alipoanza kufundishwa mziki mpaka
kuanza kutengeneza pesa kupitia ngoma na album alizowahi kuachia.
Amini aliagwa
THT baada ya kupata mkataba wa kibiashara na kampuni ya BME (Blast
Morden Entertainment) ambayo imemtengea shilingi milioni 46 kwa ajili
ya kazi zake kuanzia audio, video, mavazi, social media na kila
kinachohusiana namziki wake. Amini ni msanii wa kwanza kusainiwa
nakampuni hiyo kama ilivyokuwa kwa Lina ambae nae aliagwa baada ya
kusainiwa na kampuni inayoitwa NFZ (No Fake Zone) na kuwa msanii wa
kwanza kwenye kampuni hiyo
Mkurugenzi
wa kampuni hiyo bwana Newton amesema ameanza na Amini kwasababu ni
msanii anaejieelewa ana displine na ni mtunzi na muimbaji mzuri.
"tumepanga kumfanyia kazi nzuri za kumuendeleza kimuziki kufanya udio na
video nzuri kumtangaza kimataifa.....
kwa
mimi tumeamua kuweka kwanza 48 millioni lakini mpaka sasa tumeshaweka
fungu la milioni 30 ambalo tumeshaanza kullitumia kwa sasa" amesema bwana Newton.. zaidi mzikilize hapo chini

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni