Bibi Cheka ashindwa kupata laki mbili kujenga kibanda anacholala - MKWELI BLOG

Karibu kwenye kitovu cha HABARI.

PATA HABARI ZA MICHEZO KUTOKA KILA KONA YA DUNIA NA MAGAZETI KWA WAKATI UKIWA KARIBU NASI

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Jumatatu, 24 Novemba 2014

Bibi Cheka ashindwa kupata laki mbili kujenga kibanda anacholala

Rapper mwenye umri mkubwa kuliko wote,  bibi cheka, wiki iliyopita kupitia 255 alifunguka kuhusu afya yake na kutuhabarisha kuwa anaumwa na ameanza kurudi katika hali yake, baada ya kuanguka ghafla miezi mitatu iliyopita.
Bibi cheka pia akatuonjesha ladha ya ngoma yake mpya ambayo anytyme label yake ya Mkubwa na Wanae wataiachia.
 kama unavyofahamu umaarufu zaidi unahitaji usalama zaidi, lakini mazingira anayoishi bibi cheka pande za Bunju jijini Dsm, ni kwenye kichumba cha udongo, ambacho anatamani kukivunja na angalau kujenga cha matofali ya cement
"hapo nnamabati matano ndani na  matofali yalikuwa 440, unaona, inapanda chumba kimoja tu, na mabati matano yanaweza kuwa chumba kimoja kwa mjengo wa kisasa kama huo lakini sasa sio hivyo kwafundi yuko nyumba hii ananijengea mimi laki mbili chumba kimoja, laki mbii tu....." amesema Bibi Cheka

Ndio maana kwa kusaidiana na wadau zaidi mwaka mmoja uliopita alinunua matofali kadhaa kwa ajili ya ujenzi lakini mpaka leo amekwama kufanikisha zoezi hilo
.
Bi cheka amedai licha ya kuwa na Tv, Computer lakini hana umeme nyumbani kwake.
Mi nna Tv nne lakini sina umeme, hata computer imo ndani,  ndo hivyo sasa utafanya nini we nyumba huna unajenga umeme (anacheka) we unalala chini huna huna kitanda ulalie mkeka halafu utie umeme
 


B cheka hakuishia hapo bali amezungumzia pia kuhusu kujihusisha sana kwenye mazoezi na jinsi majirani zake wanavyomchukulia

Hakuna maoni:

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Kurasa