Mshambuliaji wa Kimataifa wa Tanzania anayekiputa katika klabu ya Genk ya nchini Ubelgiji Mbwana Ally Samatta amesema bado anafikiria kucheza soka nchini za Uhaspania na Uingereza kama atatakiwa na vilabu vya nchi hizo.
Mshambuliaji wa Kimataifa wa Tanzania anayekiputa katika klabu ya Genk ya nchini Ubelgiji Mbwana Ally Samatta amesema bado anafikiria kucheza soka nchini za Uhaspania na Uingereza kama atatakiwa na vilabu vya nchi hizo.Samatta amesema klabu ya Genk inautamuduni wa kuuza wachezaji hivyo, anadhani mkataba hautokuwa shida kuvunjwa pindi akitakiwa kuuzwa.Nahodha huyo wa timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars,amesema inatakiwa uvumilivu kucheza kwenyeligi ya Ubelgiji kwa kuwa haina umaarufu sana kwa kuwa haionyeshwi sana,ukilinganisha na ligi nyingine za Ulaya.Akiulizwa kuhusu timu gani za Uhispania na Uingereza angependa kuchezea, Samatta amesemeani siri yake, na asingependa kwa sasa kuweka wazi.Samatta aliyejiunga na Genk kwa mkataba wa miaka3, mwezi Januari mwaka huu, akitokea TP Mazembe ya DR Congo, hadi sasa amefunga mabao mawili, huku akionekana kuanza kuzoea ligi hiyo inayotumia mchezo wa kasi na nguvu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni