Baada ya shirika la ufadhili la Marekani kupitia mradi wa changamoto za Milenia (MCC) kusitisha msaada wake kwa serikali ya Tanzania kwa madai ya uchaguzi wa Zanzibar na kutekelezwa kwa sheria ya makosa ya mtandao, wadau wamekuwa na maoni tofauti.
Mbunge wa Kigoma mjini kwa tiketi ya Chama Cha ACT Wazalendo, Mh Zitto Kabwe.
Mbunge wa Kigoma mjini Mh Zitto Kabwe amefunguka na kusema kuwa mzigo huo Chama ChaMapinduzi inabidi kuubeba na wasijifanye ni mzigo wa nchi.Bodi ya Shirika la Changamoto za Milenia (MCC) imesema Tanzania haijatimiza viwango vinavyohitajika ili kunufaika na ufadhili kutoka kwa shirika hilo, na hivyo basi haitapokea msaada wa awamu ya pili ambao ulikuwa wa jumla ya Dola 472.8 milioni ambazo ni sawa na shilingi trilioni mojaza Tanzania.Kabwe amedai kuwa uzalendo ni kutaka haki ya kidemokrasia Zanzibar amesema hatakubali kuvishwa koti la uzalendo kwenye suala la MCC kwani sauala hilo ni la CCM."Uzalendo ni kutaka haki ya kidemokrasia Zanzibar. Haki ya Wananchi waliochagua viongozi wao oktoba 25, 2015. Sitakubali kuvishwa koti la uzalendo kwenye suala la MCC. Hilo ni suala la CCM, kukosa misaada ya Marekani ni matokeo ya ubabe wa CCM kuhusu Zanzibar. Haina mahusiano yeyote na Uhuru wa nchi yangu. Nawasihi Wazanzibari wawe na subra Mola kamwe hatawatupa. Haki itapatikana tu. Demokrasia tu. Nawasihi Watanzania kuelewa kwamba CCM ndiyo imetufikisha hapa na iubebe mzigo huu bila kufanya ni mzigo wa Nchi". amesemaZitto Kabwe.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni