Serikali ya Rais John Magufuli imesisitiza kuwa mtumishi atakayetumia fedha za umma kusafiri nje ya nchi bila kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi Ikulu atakuwa ameingia kwenye matatizo makubwa.Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, aliliambia Nipashe kwa njia ya simu jana kuwa, serikali imeendelea kutilia mkazo agizo lake la kuzuia safari za nje ili kuokoa fedha nyingi zilizokuwa zikitumika.“Bado hatujalegeza masharti msimamo wetu bado uko pale pale, safari za nje zisizo na tija kwa Taifa hazitakuwepo tena na ole wake atakayekiuka agizo la Ikulu,” alisema Balozi Sefue.Alisema taifa limepata tija kwa kuokoa fedha ambazo zingetumika kwa ajili ya safari zilizokuwa zimepangwa kufanywa kuanzia mwezi Novemba mwaka jana.Kwa mujibu wa taarifa aliyoitoa Balozi Sefue wakati akizungumzia siku 100 za Rais Magufuli Ikulu, serikali iliokoa kiasi cha Sh. bilioni 7 ndani ya siku hizo alizokaa madarakani.“Kiasi hiki cha fedha kiliokolewa kuanzia Novemba hadi Desemba tu kwa sababu mwezi wa Oktoba RaisMagufuli hakuwa ameanza kazi," alisema Sefue.Novemba 6 mwaka jana, Rais Magufuli, alitoa waraka wa kufuta safari zote za nchi ya nchi kwa watumishi wote wa umma.Masharti ya safari za nje yaliyotolewa ni kuomba kibali kwa Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Sefue na baadae kibali hicho huwasilishwa kwa Msajili wa Hazina kabla ya kwenda kwa Katibu Mkuu wa Wizara husika ili ajenge hoja ya umuhimu na tija itakayopatikana katika safari husika.Waraka huo pia ulimtaka Mtendaji Mkuu wa Shirika au taasisi kupima maombi ya safari husika, ili kuona kama yana tija au umuhimu wa kuombewa kibali kwa Katibu Mkuu Kiongozi, kabla ya kuwasilishwa kwa Msajili wa Hazina.Masharti hayo ya safari yanavipengele vitano ambavyo vinatakiwa kuzingatiwa wakati wa kuwasilisha hoja ya safari ambapo kipengele cha kwanza ni chanzo cha safari husika, faida yake, nini umuhimu wa safari hiyo na isipofanyika madhara yake kwa taifa.Pia kipengele cha gharama za safari, kimeweka masharti yanayomtaka mwombaji aainishe gharama ya tiketi ya ndege, posho za safari husika, mlipaji wa gharama za safari na uwezo wa taasisi kifedha.Kwa kipengele cha tano cha sharti la nne kinamtaka mwombaji aeleze manufaa ya safari hiyo kwa taasisina taifa kama imewahi kufanyika huko nyuma.Ili kuonyesha kuwa tamko la kupiga marufuku safari hizo halikuwa la mzaha, watumishi wanne wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), waliosafiri nje ya nchi bila kibali cha Ikulu walisimamishwa kazi mwishoni mwa mwaka jana.Waliosimamishwa kazi ni watumishi waandamizi wa taasisi - Msemaji wa Takukuru, Doreen Kapwani, Mary Mosha, Ekwabi Mujungu na Rukia Nikitas.
Post Top Ad
Responsive Ads Here
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Post Bottom Ad
Responsive Ads Here
Author Details
Templatesyard is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates which are professionally designed and perfectlly seo optimized to deliver best result for your blog.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni