Matokeo mabaya kidato cha nne. - MKWELI BLOG

Karibu kwenye kitovu cha HABARI.

PATA HABARI ZA MICHEZO KUTOKA KILA KONA YA DUNIA NA MAGAZETI KWA WAKATI UKIWA KARIBU NASI

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Jumamosi, 20 Februari 2016

Matokeo mabaya kidato cha nne.

Baraza la Taifa la Mitihani Tanzania (Necta), limetangaza matokeo ya mtihani wa kidato cha nne uliofanyika Novemba 2015, ambayo yanaonyesha takriban asilimia 75 ya watahiniwa, wamefanya vibaya.Katika matokeo hayo, wanafunzi waliopata daraja la kwanza hasdi la tatu ni asilimia 25 wakati asilimia 74.66 wamepata daraja la nne na sifuri.Akizungumza na Nipashe baada ya kutangaza matokeo hayo jana, Katibu Mtendaji wa Necta, Dk Charles Msonde, alisema bado hali ni mbaya kwa kuwa ilitakiwa waliopata daraja la kwanza hadi la tatu wawe angalau asilimia 50.“Bado ufaulu kwenye masomo mengi haujafika asilimia 50, ndiyo maana  daraja la nne linakuwa na karibu asilimia 42. Ukiona daraja la kwanza mpaka la tatu ni asilimia 25, ujue hali ni mbaya.“Waliofaulu daraja la kwanza mpaka la tatu ndio wanaotakiwa kwenda kidato cha tano. Hawa wangetakiwa wawe wengi, tungepata kama asilimia 50 waliopata daraja la kwanza mpaka la tatu, tungekuwa tumepiga hatua.“Kwa sababu ya hali hii, ufaulu wa masomo mengi hauvuki asilimia 50. Ni  masomo machache sana ufaulu umevuka asilimia 50,” alisema Dk. Msonde.Ubora wa ufauluKuhusu ubora wa ufaulu, Dk. Msonde alisema wanafunzi waliopata daraja la kwanza ni 9,816 sawana asilimia 2.77, kati yao wavulana ni 5,973 (asilimia3.46) na wasichana 3,843 sawa na asilimia 2.11.Alisema watahiniwa 31,986 sawa na asilimia 9.01 walipata daraja la pili, kati yao wavulana ni 19,791 (asilimia 11.460 na wasichana 12,195 (asilimia 6.69).Dk. Msonde alisema watahiniwa waliopata daraja la tatu ni 48,127 sawa na asilimia 13.56. kati yao, wavulana ni 27,749 (asilimia 30.99) na wasichana ni 20,378 (asilimia 11.18).Watahiniwa waliopata daraja la nne ni 151,067 sawa na asilimia 42.57, kati yao wavulana ni 71,358 ambao asilimia 41.32 na wasichana 79,709 sawa na asilimia 43.75.Matokeo hayo yanaonyesha kuwa waliopata daraja sifuri ni 113,489 (asilimia 32.09) ya watahiniwa wote waliofanya mtihani. Kati yao, wavulana ni 47,812 ambao ni asilimia 27.69 na wasichana 63,841 sawa na asilimia 35.04.“Matokeo haya yanaonyesha kati ya wanafunzi waliopata ufaulu mzuri wa daraja la kwanza mpaka la tatu ni 94,941 sawa na asilimia 24.73, wasichana wakiwa ni 38,338 sawa na asilimia 19.63 na wavulana 56,603 sawa na asilimia 29.99,” alisema Dk. Msonde.Ufaulu wa jumlaAkizungumzia ufaulu kwa ujumla wake, alisema watahiniwa 272,947 sawa na asilimia 67.53 ya watahiniwa wasichana 131,913 sawa na asilimia 64.84 na wavulana wakiwa 141,034 sawa na asilimia71.09 wamepata daraja la kwanza hadi la nne. Alisema waliopata daraja la nne, kimsingi huwa hawapati nafasi za kuendelea na kidato cha tano.“Mwaka 2014 watahiniwa 196,805 sawa na asilimia 68.33 walifaulu kwa kiwango cha daraja la kwanza mpaka la nne, hivyo ufaulu wa jumla wa mwaka huu umepungua kwa asilimia 0.80, ukilinganishwa na ule wa mwaka 2014,” alisema.Kwa upande wa watahiniwa wa shule waliofaulu ni 240,996 sawa na asilimia 67.91 ya waliofanya mtihani huo, wasichana wakiwa 131,913 (asilimia 64.84) na wavulana 141,034 (asilimia 71.09).“Mwaka 2014 watahiniwa wa shule waliofaulu walikuwa 167,643 sawa na asilimia 69.76 ya watahiniwa wote wa shule, hivyo ufaulu wa shule kwa mwaka jana umeshuka kwa asilimia 1.85 ikilinganishwa na mwaka 2014,” alisema Dk. Msonde.Matokeo makubwa sasaSerikali ya awamu ya nne, baada ya asilimia 60 ya wanafunzi waliofanya mtihani wa kidato cha nne mwaka 2012 kupata sifuri, ilijiwekea malengo ya kupandisha ufaulu kupitia mpango wa Maendeleo Makubwa Sasa (BRN).Katika Mpango huo, serikali ilipanga kupandisha ufaulu wa jumla kutoka asilimia 43, iliyopatikana baada ya kufutwa kwa matokeo ya awali na kupangwa upya mpaka asilimia 60 mwaka 2013. Ilijipangia pia kufikisha ufaulu kwa asilimia 70 mwaka 2014 na asilimia 80 au zaidi mwaka jana.Katika kufikia lengo hilo, upangaji wa madaraja ulibadilishwa kutoka kwenye mfumo wa madaraja kwenda GPA.WatahiniwaAkitangaza matokeo hayo, Dk. Msonde alisema watahiniwa 448,382, wasichana wakiwa 229,144 (asilimia 51.10) na wavulana 219,238 ( asilimia 48.90), waliosajiliwa kufanya mtihani huo, lakini waliofanya ni 433,633 sawa na asilimia 96.71%). Walioshindwa kufanya 14,749 (asilimia 3.29).Alisema watahiniwa wa shule waliosajiliwa walikuwa 394,065 lakini  waliofanya mtihihani ni 384,300 (asilimia 97.52) wasichana wakiwa  195,413(asilimia 97.22)  na wavulana 188,887 ( asilimia 97.83).  watahiniwa 9,765 sawa na asilimia 2.48 hawakufanya mtihani.Kwa upande wa watahiniwa wa kujitegemea, alisemawaliosajiliwa walikuwa 54,317. Kati  yao 49,333 (asilimia 90.82) walifanya mtihani huo ilhali   4,984 (asilimia 9.18) hawakufanya.Dk Msonde alisema watahiniwa wa mtihani wa maarifaa (QT) walikuwa  7,536 sawa na asilimia 46.59 wakati mwaka 2014 walikuwa 6,810 sawa na asilimia 55.29.Ufaulu kwa masomoDk Msonde alisema ufaulu wa watahiniwa wa shule kwenye masomo ya elimu ya uraia (Civics), Historia, Jografia, Kiswahili, Kingereza, Kemia, Baiolojia na masomo ya biashara (Commerce na Book-keeping) umepanda kati ya asilimia 1.09 na 12.86 ikilinganishwa na mwaka 2014.“Ufaulu wa juu kabisa ni ule wa somo la Kiswahili. Asilimia 77.63 ya watahiniwa wote wa shule waliofanya somo hilo wamefaulu, huku ufaulu wa chini kabisa ukiwa ni kwenye somo la Hisabati  kwani asilimia 16.76 ya watahiniwa ndio waliofaulu,”alisema.Tathimini ya matokeoDk Msonde alisema katika matokeo ya jumla kwa watahiniwa wa shule, idadi ya waliofaulu imeshuka kwa asilimia 1.85 kutoka asilimia 69.76 mwaka 2014hadi asilimia 67.91 mwaka jana.“Takwimu za matokeo zinaonyesha bado ufaulu wa masomo mengi ni chini ya asilimia 50 na watahiniwawaliopata daraja la kwanza mpaka la tatu ni robo ya watahiniwa wote waliofanya mtihani. Kwa hiyo, juhudi za makusudi ili kuinua kiwango cha ufaulu wamasomo yote,” alisema.Matokeo yaliyozuiwaWatahiniwa 23 waliopata matatizo ya kiafya na kushindwa kufanya baadhi ya masomo, matokeo yaoyamezuiwa na watatakiwa kumalizia masomo ambayo hawakufanya kwenye mtihani wa mwaka huu.Alisema watahiniwa wengine 98 walishindwa kufanya mitihani yote kwa sababu za kiafya na mwaka huu wataruhusiwa kufanya mtihani huo.Aidha, Dk. Msonde alisema baraza limefuta matokeo ya watahiniwa 87 walifanya udanganyifu kwenye mitihani. Kati yao 25 ni wa kujitegemea, 52 wa shule na 10 wa QT.Watahiniwa 20 boraButogwa Shija kutoka shule ya Canossa ya Dar es Salaam, ameongoza katika wanafunzi 10 bora akifuatiwa na Congcong Wang wa Shule ya Wasichana ya Feza pia ya Dar es Salaam. Innocent Lawrence wa Shule ya Wavulana ya Feza ameshika nafasi ya tatu.Wengine kuanzia namba nne na shule zao kwenye mabano ni Dominick Aidano (Msolwa, Morogoro), Sang’udi Sang’udi (Ilboru, Arusha), Asteria Chilambo na Belinda Magere (wote Canossa), Humfrey Kimanya (Msolwa), Bright Mwang’onda na Erick Mwang’ingo (wote Marian Boys).Mwalimu wa Mwanafunzi BoraMkuu wa Shule ya Canossa, Irene Nakamanya, alisema siri ya Butogwa  aliyeongoza kitaifa na wenzake wawili walio kwenye 10 bora kufanya  vizurini nidhani na kusali sana.“Kwa kweli naona kama Mungu kajibu maombi yao. Wao na mwenzao mmoja ambaye kwenye kundi la 10 bora hayumo, walikuwa wanasoma sana, wana nidhamu ya hali ya juu na walikuwa wanasali sana,” alisema.Alisema Shija tangu kuanza kidato cha kwanza shuleni hapo, alikuwa akishika kati ya nafasi ya kwanza na ya tatu ingawa mara nyingi alikuwa wa kwanza.Wasichana 10 boraKwa mujibu wa matokeo hayo, wasichana 10 bora, mbali na Butongwa Shija, Congcong Wang, Asteria Chilambo ni Belinda Magere (Canossa),  Lilian Kiwone na Marynas Duduye (St. Francis ya Mbeya), Julieth Mbalilaki (Baobab ya Pwani), Vaileth Lazaro (Kilakala ya Morogoro), Nancy Shao (Canossa) na Emmy Shemdangiwa kutoka St. Mary’s Mazinde Juu,Tanga.Wavulana 10 boraWavulana 10 bora ni Innocent Lawrence (Feza Boys, Dar es Salaam), Daminick Aidano (Msolwa), Sang’udi Sang’udi (Ilboru), Humphrey Kimanya (Msolwa), Bright Mwang’ingo, Erick Mwang’ingo na Mohamed Kingume ( wote Marian Boys, Pwani).Wengine ni David Joseph (Ilboru), Daniel Mabimbi (Alliance Boys ya Mwanza) na William Kihanza (Mzumbe, Morogoro).Shule 10 boraKatika kundi la Shule 10 bora, zile za serikali zimetupwa ambapo hakuna hata moja iliyoingia kwenye kundi hilo.Shule zilizofanya vizuri na mikoa yake kwenye mabano ni Kaizirege (Kagera), Aliance Girls (Mwanza), St Francis Girls (Mbeya), Alliance Boys (Mwanza), Canossa (Dar es Salaam), Marian Boys (Pwani), Alliance Rock Army (Mwanza), Feza Girls na Feza Boys (Dar es Salaam) na Uru Seminary (Kilimanjaro).Shule  10 za mwishoKatika kundi la shule 10 za mwisho na mikoa yake kwenye mabano iliyovuta mkia ni Pande (Lindi), Igawa (Morogoro) Korona (Arusha), Sofi (Morogoro),Kurui (Pwani), Patema (Tanga), Saviak (Dar es Salaam), Gubali (Dodoma), Kichangani na Malinyi (Morogoro).

Hakuna maoni:

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Kurasa