Majaliwa anusa harufu ya ufisadi Bandari Mtwara. - MKWELI BLOG

Karibu kwenye kitovu cha HABARI.

PATA HABARI ZA MICHEZO KUTOKA KILA KONA YA DUNIA NA MAGAZETI KWA WAKATI UKIWA KARIBU NASI

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Jumatatu, 29 Februari 2016

Majaliwa anusa harufu ya ufisadi Bandari Mtwara.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, amekutana na ufisadikatika utoaji wa zabuni wa ujenzi wa gati mpya tatu Bandari ya Mtwara.Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na Ofisi ya Waziri Mkuu kwa vyombo vya habari jana, ufisadi huo alikutana nao Jumamosi iliyopita wakati akiwa kwenye ziara bandarini hapo, akikagua eneo la ujenziwa gati hizo.Taarifa hiyo ilisema, Majaliwa alieleza ana taarifa kuhusu utolewaji wa zabuni hiyo na mzabuni ameshashinda lakini kuna madai kwamba watu wa manunuzi kupitia Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA) ndiyo wanakwamisha zabuni hiyo.Kutokana na hilo, Waziri Mkuu aliwataka wabunge wa mkoa wa Mtwara washirikiane kusimamia suala hilo ili ujenzi wake uweze kuanza mara moja na kuzalisha ajira kwa wananchi wa mkoa huo.“"Ujenzi ukikamilika siyo tu ajira zitaongezeka, bali hata meli nyingi zitaleta mizigo katika bandari hii na mapato ya mkoa yataongezeka,” ilisema taarifa hiyo ikimnukuu Waziri Mkuu na kuongeza:“Natambua kwamba kuna mpango wa kujenga gati nne, ambazo moja kati ya hizo itajengwa na TPA (Mamlaka ya Bandari), lakini hizi tatu zilitangazwa na kupata mzabuni ambaye ni kampuni ya Hyundai kutoka Japan lakini imekuwa ikizungushwa bila sababu. Tutafuatilia kubaini tatizo liko wapi.”“Sasa hivi tuna uwezo wa kupaki meli moja tu, lakini gati hizi zikikamilika tutaweza kuwa na meli tatu kwampigo, cha msingi tusimamie maamuzi yetu kwambalazima wafanyabiashara wa korosho watumie bandari hii kusafirisha mizigo yao na si kuipeleka kwingine.”‘

MAJIPU’ BODI YA KOROSHO
Waziri Majaliwa alisema kwenye Bodi ya Korosho nako kuna majipu yanahitaji kutumbuliwa.“RCC (Kamati ya Ushauri ya Mkoa) ilishakaa na kupitisha uamuzi kuwa mizigo yote ipitie Bandari ya Mtwara, lakini kuna watu ndani ya bodi hiyo wanatoavibali vya kusafirisha mizigo kupitia Bandari ya Dar es Salaam,” alisema.Alimtaka Mkuu wa Bandari ya Mtwara, Prosper Kimaro, awe makini na watu wa kitengo cha manunuzi katika bandari hiyo kwa sababu ni chanzo cha upotevu wa fedha za serikali kutokana na watu wachache."Hapa si kuna mtu alitaka kuiba Sh. milioni 300 kwa kufoji saini za wakubwa wake?” alihoji Waziri Mkuu swali ambalo lilijibiwa na Kimaro kwamba ni kweli lakini uongozi uliingilia kati kabla wizi huo haujakamilishwa.

FIDIA
Kuhusu fidia kwa wakazi wa vijiji vya Kisiwa na Mgao ambao wamekubali kuhama ili kupisha upanuzi wa bandari hiyo, taarifa hiyo ilisema Waziri Mkuu alisema tayari  Sh. bilioni 13.8 zimekwishatengwa na wizara na zitatolewa mwezi ujao.Taarifa hiyo ilisema Majaliwa alimtaka mkuu wa mkoa huo akae na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa, ili kuweka mbinu za kuthibiti upenyo wa uingizaji wa mchele na sukari kwenye bandari bubu kwa lengo la kukwepa kodi.Desemba 3, mwaka jana Waziri Mkuu alifanya ziara ya kushutukiza katika Bandari ya Dar es Salaam na kukuta makontena 2,431 yalitolewa bila kulipiwa ushuru, pamoja na Novemba 27, mwaka jana kubainiutoroshwaji wa makontena  349 ambayo hayakulipiwa kodi na kuisababishia serikali hasara ya Sh. bilioni 14.Aidha, Februari 19, mwaka huu, kiongozi huyo alifanya ziara ya kushtukiza katika  Bandari ya Tanga na kukuta matishari tatu zikiwa chakavu, bila injini wakati serikali ilitoa fedha ya ununuzi wa matishari ya kisasa.

Hakuna maoni:

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Kurasa