Baraza la Madiwani lafuta posho za vikao - MKWELI BLOG

Karibu kwenye kitovu cha HABARI.

PATA HABARI ZA MICHEZO KUTOKA KILA KONA YA DUNIA NA MAGAZETI KWA WAKATI UKIWA KARIBU NASI

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Jumatatu, 29 Februari 2016

Baraza la Madiwani lafuta posho za vikao

BARAZA la Madiwani la Halmashauri ya Jiji la Mbeya limeazimia kuondolewa kwa matumizi ya fedha yasiyokuwa ya lazima, imeelezwa.Hatua hiyo ni pamoja na kufuta  baadhi ya posho za vikao na chakula kwa wajumbe.Baraza pia limeazimia  kuanza kutumia vema fedha hizo ikiwamo kupunguza changamoto mbalimbali zamaendeleo zinazowakabili wananchi hususan katika elimu, afya, maji  na miundombinu ya barabara.Azimio hilo lilifikiwa jana katika kikao maalumu cha kujadili na kupitisha bajeti ya fedha ya mwaka 2016/2017 kilichafanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa halmashauri ya jiji hilo.Meya wa Jiji la Mbeya, David Mwashilindi, alisema ilihalmashauri iweze kutoa huduma bora kwa wananchi  ni vema matumizi ya fedha yasiyokuwa na lazima yakapunguzwa kama posho za baadhi ya vikao na chakula kwa wajumbe.“Halmashauri yetu inakabiliwa na changamoto nyingi za elimu, afya, maji na miundombinu ya barabara.“Ukiangalia kuna baadhi ya matatizo kama vile uhaba wa matundu ya vyoo, ukarabati wa majengo ya shule yapo ndani ya uwezo wetu ni vema tukapunguza matumizi ya fedha yasiyokuwa na ulazima katika kuyatimiza haya,”alisema Meya.Alisema haiwezekani wajumbe wakaketi kwenye kikao kwa  saa sita au  tano na kulipana posho na kula chakula ambacho kinatumia fedha wakati watoto shuleni wanakaa chini na kutumia vyoo ambavyo miundombinu yake ni mibovu na ni hatari kwa maisha yao.Jukumu la madiwani na watendaji wa serikali ni kuhakikisha wanasimamia  ujenzi na uboreshaji wa miundombinu ya shule za msingi na sekondari, hususan kuongeza matundu ya vyoo, madawati,madarasa, uwekaji wa sakafu, milango na madirisha.Akizungumzia suala hilo, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya jiji la Mbeya, Dk. Samweli Lazaro, aliwataka madiwani hao kuhakikisha wanaondoa tofauti za  siasa katika kutekeleza majukumu ya maendeleo.Alisema  lengo la Serikali ni kuhakikisha wanananchiwote wananufaika sambamba na kukuza Pato la Taifa.

Hakuna maoni:

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Kurasa