Wabunge wapania muswada mafisadi - MKWELI BLOG

Karibu kwenye kitovu cha HABARI.

PATA HABARI ZA MICHEZO KUTOKA KILA KONA YA DUNIA NA MAGAZETI KWA WAKATI UKIWA KARIBU NASI

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Alhamisi, 14 Januari 2016

Wabunge wapania muswada mafisadi

Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wamesema wanasubiri kwa  hamu muswada wa kuanzishwa kwa Mahakama Maalum ya kushughulikia mafisadi kama iliyoahidiwa na Rais John Magufuli.Wakizungumza na Nipashe jana, baadhi ya wabunge hao walisema wanausubiri Muswada huo kwa hamu ili waupitishe kwa ajili ya kuanzishwa kwa mahakama hiyo itakayosaidia kuharakisha kesi za mafisadi.Mbunge wa Jimbo la Manonga, mkoa wa Tabora, Seif Gulamali (CCM), alisema wanatarajia serikali itapeleka muswada huo kwa ajili ya kutajwa, kuujadili na kuupitisha kwa manufaa ya wananchi kwani unaweza kutatua kero ya ufisadi, rushwa na matumizi mabaya ya fedha za serikali.Alisema mahakama ya aina hiyo ni muhimu katika kupambana na watu wanaojinufaisha kwa kupora mali za Watanzania.“Sisi kama wabunge bila kujali itikadi za vyama, tunausubiri kwa hamu muswada huo uletwe bungeni ili tuujadili na kuupitisha ili uwe sheria na hatimaye mahakama inayosemwa semwa ianzishwe na ianze haraka,” alisema Gulamali.Alisema anatambua namna ambavyo Rais Magufuli anakerwa na wizi unaofanywa na baadhi ya watumishi wa serikali na kwamba kuwasilishwa kwa muswada huo utakuwa kama mwarobaini wa tatizo hilo.“Tutamuunga mkono Rais kwa jambo hili, natambua ameguswa na sisi kama wabunge tuna wajibu wa kuusubiri muswada huo katika kikao kinachokuja tuweze kutekeleza kazi walizotutuma wananchi,” aliongeza.Mbunge wa Lulindi, Jerome Bwanausi (CCM), alisema katika mchakato wa uanzishwaji wa chombohicho, lazima wabunge waondoe itikadi ya vyama vyao na wamuunge mkono Rais Magufuli kuhakikisha muswada unapitishwa haraka.“Suala la ufisadi halina chama, lazima tukubaliane utakapoletwa tuusome na kuuelewa na kuchukua uamuzi utakaowafanya wananchi wetu wafurahi maana tatizo la ufisadi limekuwa kero kwa kila mtu na nadhani wananchi watafurahi sana watakaposikiatumeupitisha,” alisema.Alisema kila mbunge ana kiu ya kuona muswada huounafikishwa haraka bungeni kama ambavyo Rais Magufuli amekuwa akijinadi kwenye kampeni zake na bunge hilo litaweka historia kwa kuujadili na kuupitisha kwa kura nyingi.Mbunge wa Iringa Mjini Mchungaji Peter Msigwa (Chadema), alisema anasubiri kuona muswada huo una kitu gani kipya ambacho kitamshawishi yeye aamini unaweza kuondoa tatizo hilo la ufisadi.“Unajua nchi yetu ina sheria nyingi nzuri ambazo zingefanyiwa kazi tatizo la rushwa na ufisadi lisingetusumbua, lakini kinachotuangusha hakuna utekelezaji mzuri na ndio maana tumefika hapa tulipo,” alisema Msigwa.Msigwa alisema yeye binafsi anaona ni jambo jema, lakini inamuwia vigumu kueleza kwa kina kwa sababu hafahamu muswada huo utasema nini na sheria zake zitakuwaje.Waziri wa Katiba na Sheria, Dk. Harrison Mwakyembe, alipozungumza hivi karibuni alisema moja ya kazi aliyopewa na Rais Magufuli ni kuhakikisha Mahakama hiyo inaanzishwa mara moja.Kwenye kampeni za Uchaguzi Mkuu uliomweka madarakani mwaka huu, Dk. Magufuli alikuwa akiahidi kuanzisha Mahakama Maalum ya kushughulikia mafisadi.Dk. Magufuli alikuwa akisisitiza kuwa akiingia Ikulu atahakikisha muswada huo unawasilishwa bungeni haraka kwa ajili ya kupitishwa na kuanza kazi mara moja kwa mahakama hiyo.Alikuwa akisema kuwa nchi ni tajiri lakini imefika ilipo sasa kutokana na mafisadi wachache ambao atawashughulikia mara tu atakapoingia madarakani.

Hakuna maoni:

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Kurasa