Marubani waombewa m10/- wasome - MKWELI BLOG

Karibu kwenye kitovu cha HABARI.

PATA HABARI ZA MICHEZO KUTOKA KILA KONA YA DUNIA NA MAGAZETI KWA WAKATI UKIWA KARIBU NASI

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Jumapili, 24 Januari 2016

Marubani waombewa m10/- wasome

Chuo cha Usafirishaji cha Taifa (NIT), kimesema gharama ya kumsomesha mwanafunzi wa urubani na wahandisi wa ndege ni Sh.milioni 10 hivyo kimeiomba serikali kupitia Bodi ya Mikopo iweze kuwasaidia wanafunzi wanaochukua kozi hizo.Hayo yalibainishwa mwishoni mwa wiki na Mkuu wa Chuo cha Usafirishaji Mhandisi Dk. Zacharia Mganilwa, wakati wa uzinduzi wa 'Banda' la ndege litakalotumika katika mafunzo ya wahandisi wa ndege na marubani.Alisema gharama hizo ni kubwa kulinganisha na kozinyingine zinazotolewa hapa nchini.Alisema Bodi ya Mikopo imekuwa ikitoa mkopo usiozidi Sh. milioni 1.5 kwa mwanafunzi ambaye adayake ni Sh. milioni kumi.Mganilwa alisema gharama kubwa zimekuwa zikibebwa na mzazi, zaidi ya Sh. milioni tisa.“Sh. milioni tisa ambazo anatakiwa alipe mzazi imekuwa kwa kiasi fulani changamoto kwao hivyo ninaomba bodi ya mikopo iweze kuliangalia suala hili, waongezewa hata kidogo,” alisema.Mganilwa aliongezea kuwa kwa hivi sasa marubani wengi na wahandisi wa ndege wamezeeka na wengine kustaafu hivyo kuiacha sekta ya anga kuwa na Watanzania wachache na wengi wageni.“Mipango na mikakati yetu mikubwa ni kuona tunazalisha watanzania wengi kabisa katika eneo hilila mafundi wa ndege na marubani, hatutaki kuachia wageni tu waweze kuajiliwa katika sekta hii ya anga nchini,” alisema.Akizungumza kwenye hafla hiyo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Faustine Kamuzola, alisema serikali itatoa kila aina ya msaada kwa NIT ili kiweze kuzalisha marubani nawahandisi wa ndege wa kutosha katika kukuza sektaya anga nchini.Profesa Kamuzola alisema serikali itashirikiana na Sekta binafsi katika kukisaidia chuo hicho kiweze kufikia malengo yake ya uzalishaji wa rasilimali watukatika sekta ya usafirishaji.“Tumesikia kutoka kwa mkuu wa chuo hiki kuwa adaya kumfundisha rubani wa ndege ama mhandisi ni Sh. milioni kumi, lakini tukimpeleka mwanafunzi nje ya nchi tutapaswa kulipa ada ya zaidi ya Sh. milioni 100, sasa serikali imewasikia,” alisema.Aliongeza kuwa kwa kutoa mafunzo haya kwa gharama ya bei nafuu kabisa, ana imani kwamba Watanzania wengi wenye nia ya kusomea urubani nauhandisi wa ndege watajiunga na chuo hicho.

Hakuna maoni:

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Kurasa