Magufuli: Nitakula sahani moja na mafisadi - MKWELI BLOG

Karibu kwenye kitovu cha HABARI.

PATA HABARI ZA MICHEZO KUTOKA KILA KONA YA DUNIA NA MAGAZETI KWA WAKATI UKIWA KARIBU NASI

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Ijumaa, 22 Januari 2016

Magufuli: Nitakula sahani moja na mafisadi

Rais John Magufuli amesema nchi yetu ni tajiri na inarasilimali nyingi ila baadhi ya matajiri ambao ni mafisadi ndio wanasababisha ionekana maskini jambo ambalo ameahidi kula nao sahani moja.Aliyasema hayo jana wakati akizungumza na wananchi wa Mkoa wa Arusha waliojitokeza  barabarani kumpokea huku wakimuomba aendelee kutumbua majipu.Alisema Tanzania inarasilimali nyingi ikiwamo Tanzanite bali kuna baadhi ya matajiri ambao wanapenda kujilimbikizia mali na wamekuwa wakifanya ufisadi na kusababisha baadhi ya wananchi kuendelea kuwa maskini pamoja na nchi yetu.“Nasema hivi, kuanzia sasa nipo tayari kulala mbele na mafisadi wote na pia nawapa onyo kali wale walimu ambao bado wanatoza ada shuleni, iwapo nitagundua mwalimu yeyote  anayetoza hela naahidi nitalala naye mbele, na katika hili,  sitalifanyia masihara hata kidogo,”alisema Magufuli.Aidha, aliwaambia wananchi kuwa kuanzia sasa elimu ni bure kuanzia shule ya msingi hadi sekondarina serekali imeshaweka mipango hiyo tayari na imeanza kutumika.Magufuli aliwasihi wananchi wa Mkoa wa Arusha na Tanzania kwa ujumla kuendelea kufanya kazi na kusema kuwa wakati wa kampeni umeisha, mambo ya siasa yameisha sasa hivi ni wakati wa kufanya kazi tu na sio kitu kingine.“Nasema hivi sasa hivi ni wakati wa kufanya kazi,  nitaendelea kutumbua majipu kila mahali na sitamuonea huruma mtu yeyote mimi kazi yangu kubwa ni kufanya kazi tu. Wananchi napenda kuwaambia fanyeni kazi kwani hapa ni kazi tu,”alisema Magufuli.Pia, aliongeza kuwa katika suala la barabara pia ataendelea kuliangalia na kufuatilia kama jinsi alivyokuwa anafanya alivyokuwa waziri.Aidha, Magufuli aliomba wananchi wamweke katika maombi kila wakati wanapokuwa katika sala zao.

Hakuna maoni:

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Kurasa