"Ni kweli kuna madhehebu mengi ya dini duniani, lakini kanisa katoliki ndilo lenye kiongozi mkuu duniani na ameonyesha uwezo mkubwa katika kupigania haki za binadamu na mabadiliko ya kiutawala kufanyika kwa njia ya amani."
Chama cha Wananchi (CUF) kimesema kimeamua kumuomba Kiongozi Mkuu Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis, kuingilia kati mkwamo wa uchaguzi mkuu Zanzibar, baada ya kuona Chama Cha Mapinduzi (CCM) hakitaki mabadiliko ya utawala kufanyika kwa njia ya amani.Hayo yalisemwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa chama hicho, Ismail Jussa Ladhu, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa jana juu sababu za kumtaka kiongozi huyo mkuu wa kidini kuingilia mgogoro huo wa uchaguzi mkuu Zanzibar.Alisema Papa Fransis ana ushawishi mkubwa katikakutetea haki za binadamu na mabadiliko ya kiutawala kufanyika kwa njia ya amani, ndiyo maanaCUF ina amini anaweza kutumia ushawishi wake kusadia tatizo la uchaguzi huo.“Papa Fransis tangu aliposhika wadhifa huo ameonyesha uwezo mkubwa katika kupigania haki za binadamu na kuona mabadiliko ya kiutawala yakifanyika kwa amani bila ya watu kupoteza maisha. Ushawishi wake katika kupigania haki za binadamu na kufanyika mabadiliko kwa njia ya amani ndiyo sababu kubwa ya kumtaka kuingilia mgogoro wa uchaguzi wa Zanzibar,” alisema na kuongeza:“Ni kweli kuna madhehebu mengi ya dini duniani, lakini kanisa katoliki ndilo lenye kiongozi mkuu duniani na ameonyesha uwezo mkubwa katika kupigania haki za binadamu na mabadiliko ya kiutawala kufanyika kwa njia ya amani.”Hata hivyo, alisema tangu Papa Fransis alipoandikiwa barua hiyo Novemba 25, mwaka jana bado chama hicho hakijapoke majibu yake, lakini wana amini itakuwa imemfikia.Alisema barua hiyo ilitumwa kupitia ubalozi wa Vatican jijini Dar es Salaam, baada ya Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha, kufuta matokeo ya uchaguzi mkuu Oktoba 28, mwaka jana na kusababisha mgogoro wakisiasa Zanzibar.Jussa alisema CUF kinaamini kuwa, mabadiliko ya kiutawala Zanzibar yatapatikana kwa njia ya amani, ndiyo maana juhudi za mazungumzo ya kidiplomasia zinandelea kufanyika sambamba na mazungumzo ya viongozi wa kitaifa Zanzibar.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni