BusinessCopy Cat yaanzisha teknolojia mkombozi kwa wafanyabiashara. - MKWELI BLOG

Karibu kwenye kitovu cha HABARI.

PATA HABARI ZA MICHEZO KUTOKA KILA KONA YA DUNIA NA MAGAZETI KWA WAKATI UKIWA KARIBU NASI

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Jumanne, 19 Januari 2016

BusinessCopy Cat yaanzisha teknolojia mkombozi kwa wafanyabiashara.

Kampuni ya Copy Cat imeanzisha teknolojia iitwayo Ricoh itakayowasaidia wafanyabiashara wakubwa na wadogo na kampuni nchini, kuokoa muda na gharama za matumizi kwa wakati husika, hatua inayolenga kuongeza ufanisi.Kadhalika, teknolojia hiyo inampa unafuu mtumiaji wa kompyuta uwezo wa kuidhibiti kwa kuweka namba za siri kuhakikisha huduma za kuchapa (printing) na huduma nyingine zinazopatikana katika ofisi yake zinakwenda vizuri.Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo, Mike Holtham, aliyasema hayo wakati akielezea umuhimu wa teknolojia hiyo inavyokuwa na manufaa katika biashara, Teknolojia ya Habari, viwandani, mfumo wa mtandano pamoja na huduma katika kampuni.Alisema kampuni ya Copy Cat ina uzoefu wa zaidi yamiaka 20 ya utendaji kazi mzuri kwa nchi za Afrika Mashariki katika masuala ya Teknolojia ya Habari, maofisini, masuala ya ushauri na masuala ya kompyuta kwa wafanyabiashara.“Ricoh ni teknolojia ya kiulimwengu ambayo inajihusisha na masuala ya ofisini pia inasaidia kurahisisha mazingira ya ufanyaji kazi katika ofisi,” alifafanua Holtham.Aliongeza kuwa kwa wafanyabiashara wakubwa na wadogo, wanaweza kukuza bishara zao kwa kutumiateknolojia hiyo inayopatikana katika kampuni yao.

Hakuna maoni:

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Kurasa