Aliewahi kuwa Manager wa Barcelona Pep Guardiola,ammwagia misifa Lionel
Messi baada ya kuvunja rekodi ya kufunga magoli mengi La Liga na kudai
kuwa itachukua miaka 600 mtu mwingine kuja kuvunja rekodi hiyo.
Messi alitandika Hat-trick weekend iliyopita na kuvunja record
iliyowekwa na Telmo Zarra (251) miaka 60 iliyopita kwenye kitabu cha
rekodi kwa kufikisha magoli 253 kwenye La Liga.
Messi alifikisha magoli 251 jumamosi iliyopita dakila ya 21Barcelona
ilipokuwa ikicheza na Sevilla na kufikia record ya Zarra, na akaivunja
recor hiyo ndani ya dakika ya 72 kwa kuingeza goli la pili na kumaliza
hat-trick katika ushindi wa 5-1.
Guardiola, ambae alishafanya kazi na Messi kati ya mwaka 2008 na 2012
amewataka watu kumpa hongera Messi kwa alichokifanikisha kwa kuwa
amevunja record ambayo haikutegemewa kuvunjwa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni