Story
ya kwanza kusikika leo ni ile inayomhusu msanii Bibi Cheka ambapo
jumatatu alisikika kuhusu kilichomkwamisha kuvunja nyumba yake ya
udongo na kujenga ya matofali kuwa ni kiasi cha shilingi laki mbili au
tatu, ambapo ameomba Watanzania wamsaidie kutokana na hali yake kwa sasa
kuwa siyo nzuri kiafya.
Mkurugenzi wa Mkubwa na Wanawe ambaye
ndiye anamsimamia Bibi Cheka kwenye kazi za muziki amesema tayari
kamsaidia Bibi Cheka tofali na amekuwa akimsaidia mara kwa mara, hiv yo
kwa sasa kila mmoja anaweza kujitolea alichonacho kumsaidia.
Kundi la Weusi Jumamosi hii wanatarajia kufanya Show ya aina yake inayoitwa ‘Funga Mwaka na Weusi’ siku ya Jumamosi Escape One Dar, ambapo watatambulisha video zao tano siku hiyo, wasanii kama Godzilla pamoja na wengine wawili watatambulishwa kwa surprise siku hiyo.
Kwa mara nyingine tena kutoka Bongo Dar es Salaam, DJ Bulla kutoka nyumba ya Burudani Clouds FM atakuwepo wikiendi hii ndani ya Jumba la BBA Afrika Kusini kuwaburudisha washiriki wa ndani ya jumba hilo.
Leo imetimia miaka miwili tangu kufariki kwa Msanii Sharo Milionea ambapo nyumbani kwao Tanga inafanyika dua maalum ya kumuombea marehemu.
Baada ya siku 100 kupita baada ya kijana
mmoja Marekani kuuawa kwa kupigwa risasi na Askari Polisi, machafuko
makubwa yametanda Ferguson, Marekani baada ya mamia ya watu kuandamana
na kufanya machafuko makubwa wakipinga kitendo cha Mahakama kumwachia
huru Askari aliyemuua kijana huyo kwa akijitetea kuwa alifanya hivyo kwa
ajili ya kujilinda.
Watu wengi ikiwemo wasanii kama Chris Brown, Diddy, T.I, Kevin Hart na Solange Knowles wamelaani maamuzi hayo wakihusisha maamuzi ya Mahakama na ubaguzi wa rangi.
Mahusiano ya Jason Derulo
na Jordin Sparks yamevunjika ambapo Jordin kaachia albam ambayo ndani
yake kuna nyimbo ambayo ni kama amezungumzia mambo kadhaa ambayo
yametokea kwenye uhusiano.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni