Msanii na mmiliki wa studio za Switch (Switch Records), Quick Rocka na
producer Nar Real waingia ndani ya bif kubwa kiasi cha kupelekea kila
mmoja kumzuia mwenzie kutumia kazi walizowahi kufanya pamoja.
Kwa madai ya Quick, Nahreal ambae alimuamini na kumuweka katika studio
yake kwa ajili ya kufanya nae kazi ameondoka tu studio bila kuaga na
kila akijaribu kumpigia simu anamkwepa, kitu ambacho ameona ni dharau
kwake na hata baada ya kumpigia simu kwa takribani miezi mitatu kumtaka
waonane waongee lakini hakufanya hivyo.
Nahreal ambae kwa sasa amefungua studio yake mwenyewe kwa upande wake
amesema sio dharau alichokifanya bali ana familia kwahiyo alikuwa busy
tu na mambo yake.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni